Bondia Mbwana Matumla kushoto akielekezwa kupiga ngumi na Said Abdulghafoor wakatio wa mazoezi ya Matumla ya kutambulisha mpambano wake na Seleiman Shabani utakaofanyika Feb 5, 2017 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa. Picha na SUPER D BOXING NEWS.
Mabondia Mesharck Mwankemwa wa Mbeya na Mbwana Matumla wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika Feb 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Mwankemwa atapanda ulingoni na Ramadhani Shauri na Matumla atamkabili Seleiman Shabani.
Mabondia Mesharck Mwankemwa wa Mbeya na Mbwana Matumla wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika Feb 5, 2017 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Mwankemwa atapanda ulingoni na Ramadhani Shauri na Matumla atamkabili Seleiman Shabani.
Wadau wa mchezo wa masumbwi nchini wakimfuraia Bondia Mbwana Matumla wa tatu kushoto akipeana mkono na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wengine kutoka kushoto ni William Kaijage Said Abdulghafoor Juma Mbili pamoja na Chaurembo Palasa.

Na Mwandishi Wetu.

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Mbwana Matumla anataraji kupanda ulingoni tena baada ya kukaa nje ya ulingo tangia mpambano wake wa mwisho aliocheza katikas ukumbi wa Dar Live Desemba 25 mwaka 2012 alivyomsambalatisha bondia David Chalanga wa Nairobi, Kenya anarudi tena ulingoni Feb 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa kupambana na Suleimani Shabani mpambano wa raundi nane uzito wa Super Feather Weight.

Mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka likiwemo la bondia Meshack Mwankemwa atakayepambana na Ramadhani Shauri wakati Mohamed Matumla atavaana na Mfaume Mfaume na Twalibu Tuwa wa Kiwangwa Bagamoyo atavaana na Saidi Chino mpambano wa ubingwa wa Taifa raundi kumi na Husein Pendeza wa Ashanti Boxing club ya Ilala atakayevaana na Said Hamdani kutoka Mbezi Conetion.

Mkwela atazipiga na Manyi Issa mpambano wa raundi kumi kumaliza ubishi wa nani zaidi ya mabondia hao ambapo Mkwela anafundishwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Issa anaefundishwa na Amos Martin Nkondo kutoka Mbezi Connection.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: