Maureen alizaliwa na kulelewa na Mama ambaye ni kichaa wale wakuzunguka na kuokota vitu barabarani, pamoja na ukichaa wake lakini yule mama alimlea vizuri binti yake akimpa chakula mpaka alipofikia umri wa kwenda shule. Kwa bahati nzuri Maureen alipata msamaria mwema ambaye alimsomesha, ingawa yule msamaria mwema alijaribu kumchukua yule Mama na kukaa naye lakini haikusaidia. Mama yule alionekana kuchoka na kuzeeka mno kutokana na ugumu wa maisha anayopitia na hali yake ya ukichaa, alionekana kama bibi wa miaka 90, ngozi yake ilionekana kusinyaa na macho kufifia, hii yote ni kutokana na kushinda kutwa nzima akizunguka juani majalalani, masokoni na barabarani kuomba mwanae Maureen apate kitu cha kula.

Kila aliporudishwa nyumbani siku mbili alirudi mtaani kuokota makopo na kula matakataka. Pamoja na ukichaa wake lakini kila siku ilikuwa ni lazima kwenda kwenye ile nyumba alikokuwa akilelewa binti Maureen kumsalimia na kila siku alikuwa akibeba chakula kwa ajili ya binti yake.

Ili Maureen ale kile chakula ilibidi kila siku kumuwekea chakula kizuri kwenye mfuko na pale alipokuwa akiomba basi walimpa kile chakula na yeye kabla ya kula alimletea binti yake. Maisha yaliendelea hivyo mpaka Maureen alipoenda chuo ndipo Mama alibaki mpweke akizunguka zunguka tu mtaani. Kule chuoni Maureen alifanya vizuri na alipomaliza chuo alifanikiwa kupata mchumba.

Alirudi kumtambulisha kwa wale wazazi waliomlea, lakini chakushangaza tu siku aliyorudi kumtambulisha mchumba wake na Mama yake alikuepo. Kwa uoga na aibu aligoma kabisa kumtambulisha, ingawa yule mama alimng'ang'ania lakini alidanganya kuwa ni kichaa tu ambaye alizoea kumpa zawadi. Siku iliisha na mipango ya harusi ikafanyika, baada ya miezi mitatu ikafanyika harusi kubwa na ya kifahari.

Wakiwa katikati ya sherehe Maureen alishangaa kumuona mama yake anaingia akiwa amevaa nguo zake chafu vilevile, Mama alisogea mpaka mbele watu wakimshangaa akatoa mfuko wake wa chakula na kumkabidhi binti yake ili ale. Maureen aliukataa na kuanza kupiga kelele lakini kabla hajafanya chochote mume wake aliuchukua ule mfuko na kuufungua kisha kuanza kukila kile chakula.

Watu wote walishtuka na kuanza kushangaa, lakini yule bwana harusi alichukua Mic na kusema. Huyu ndiye Mama mkwe wangu, Mama mzaa chema. Najua mnamshangaa na hali yake lakini kwa hali hii hii ndiyo alimza na kumlea mke wangu na ndiye atakuwa Bibi wa watoto wangu" Kila mtu alibaki kushangaa hata yule binti alishangaa huku machozi ya kimtoka, yule kijana alimgeukia mkewe.

"Najua sababau za wewe kuficha lakini unapaswa kutambua kuwa nakupenda na nampenda mama yako kama vile ninavyompenda mama yangu. Ulimwengu mzima utamuona kichaa lakini yeye ndiye aliyekuzaa na kukufanya uwe hivi leo. Unavyoniona hivi Baba yangu alinizaa na kunitelekeza, pamoja na pesa zake akili zake lakini alinitelekeza, sasa hembu jiulize kichaa ni nani kati ya mwanaume aliyetelekeza mwanae au mama kama huyu ambaye mpaka leo anajua bado ni mtoto na anakujali kwa chakula?"

Ukumbi mzima uliibuka kwa vifijo, watu wakishangilia Maureen akiwa anatokwa na machozi alimkumbatia Mama yake, alichukua kile chakula na wote wakaanza kukila. Yule kijana ndiyo alimualika kwani siku aliyoenda kutambulishwa na kumuona alihisi kitu hivyo akaamua kufuatilia mpaka alipoujua ukweli. Alijua sababu ya mchumba wake kuficha lakini alitaka ulimwengu mzima kujua kuwa hajali na anampenda bila kujali historia yake.

HAKUNA KAMA MAMA, UPENDO WAKE HAUNUNULIWI WALA HAUPUNGUI USICHOKE KUMUAMBIA NAMNA UNAVYOMPENDA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: