Sunday, January 8, 2017

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA AWAONYA WANASIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU

Mkuu wa wilaya ya Kahama Bw. Fadhili Nkurlu, amewaonya wanasiasa wanaotumia lugha za vitjsho, kashfa na uchochezi kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani kuacha mara moja tabia hiyo.

Nkurlu aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara na kuongeza kuwa hatua kali sana zitachukuliwa kwa mwanasiasa wa chama chochote atakayesikika akitoa lugha za uchochezi au kashfa kwa viongozi wa serikali.

" kumezuka tabia ya wanasiasa kuwakashfu viongozi wa serikali. Sasa nasema hivi Mimi ndiye mkuu wa wilaya hii na ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. Sitamvumilia mtu yeyote anayetumia jukwaa la kampeni kutoa lugha zenye viashiria vya uvunjifu wa amani na kuwakashfu viongozi".

Nkurlu amewataka wanasiasa kunadi sera zao na namna wanavyoweza kuwasaidia wananchi badala ya kujikita kwenye uchochezi na kashfa kwa viongozi huku wengine wakitishia amani. Pia amewataka kufuata mwongozo na maadili ya uchaguzi. "kura hukomesha mashindano. Ni heri kunadi sera zako ili upate kura nyingi. Kukashfu kiongozi hakutakusaidia lolote badala yake unatafuta ugomvi wa makusudi na serikali. Fanyeni kampeni za kistarabu"

Hivi karibuni akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni hizo, mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha upinzani alinukuliwa akisema kwamba ataleta malori 10 ya vijana toka Tarime ili kufanya fujo endapo chama chake hakitashinda kwenye uchaguzi mdogo wa diwani kata ya Isagehe wilayani hapa utakaofanyika tarehe 23 mwezi huu.

Uchaguzi huu mdogo unafanyika baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu