Leo imenibidi niongelee kuhusu swala la Mapenzi kutokana na Kuona na kusoma post na comments za watu kuhusiana na Kijana Fredy aliyejikatisha maisha kisa binti aitwaye Rose kuchukuliwa na rafiki yake ambaye ni bosi wake bila shaka..

Hata katika Vitabu vitakatifu vinatuambia Kuwa "Kila mmoja ataubeba Msalaba wake Mwenyewe" na kama ambavyo ilivyo kuwa" “Kila mmoja wetu atatoa hesabu kwa Mungu kwa ajili yake mwenyewe.”—WAROMA 14:12. Iweje wewe leo ukaubebe Msalaba wa Mzazi wa Mwenzio wakati sio Jukumu lako? Una mgharamia wewe ni nani yake? Haya yote yanafanywa endapo tu tayari umeshaingia kwenye agano la Ndoa. Na agano la Ndoa huwa linaanzia pale unapomwambia binti kuwa "Nitakuoa" au Binti anapokwambia "Nitaolewa na Wewe" Hili ndio agano la kwanza ambalo ukinena mbele ya dunia na Mbinguni linakuwa limenenwa na ukiliandika Duniani basi na Mbinguni linakuwa limeandikwa kama ilivyo kuwa Kila lifunguliwalo duniani na Mbinguni limefunguliwa... Sasa wewe hukutamka kuoa au kuolewa na mtu fulani maana yake hakuna agano lolote au haukuniwia kufanya hivyo basi yote yatakayo tokea ni bure kabisa.

Na ndio maana Mwanaume unaposema au kumwambia mwanamke kuwa nitakuoa na bahati mbaya hukumuoa huyo bila kutubu na kuvunja agano hilo kabla ya kumuoa huyo mwingine basi tegemea mambo mengi kukutokea kwenye hiyo ndoa yako mpya kwasababu uliposema nitakuoa maana uliliandika Duniani na kila kinachoandikwa duniani basi na Mbinguni kimeandikwa. Kwa hiyo Kabla ya Kuoa mwingine basi tunapaswa kuvunja maagano hayo kwanza kwasababu Kuongea ni Lango Mojawapo.

Sasa ewe Kijana unayetaka kumsomesha, kumgharamia kwa kila kitu wakati hata kwao hukujitambulisha wala kwenu hakujitambulisha unataka nini? Huo ni msaada tu unakuwa umeutoa na sio lazima akubaliane na wewe... Ungekuwa ushalipa mahali hapo sawa tungeongea mengine ila kwasasa HUPASWI KUBEBA MSALABA AMBAO SIO WAKO... KILA MMOJA ATABEBA MSALABA WAKE MWENYEWE... WAPENZI HAWASOMESHWI NA MPENZI SIO KAZI YAKO HIO WEWE....

KUHUSU KUJIKATISHA MAISHA.

Ni kweli mapenzi yanaumiza tena sana tu na kila mmoja wetu anayesoma hapa alishawahi kuumizwa na mapenzi lakini inategemea baada ya kuumizwa nini kilifuata. Lakini kijana Fredy asionekane mjinga wala Mwendawazimu kwa kitendo cha kukatisha uhai wake laasha bali alikosa watu wa Karibu sana katika kumfanya aone tatizo lililompata sio lake peke yake ni tatizo lililowapata wengi na pia litaendelea kuwapata wengine wengi zaidi.

Sababu iliyopelekea Fredy kujiua sio Mapenzi bali ni hisia kali juu ya Yule aliyempenda kwa imani kuwa Hakuna faida ya kuishi bila ya Rose.Hii kisosholojia tunasema HIGH BELIEVE ndiyo iliyopelekea huyu kijana kujiua.

Kwa vijana wengine Eleweni kuwa tatizo kama hili likitokea kwako tena wewe sio wa kwanza wala wa mwisho na maisha yana maana kubwa sana kuliko Mapenzi.

Muda wote tunapaswa kushukuru kwa Mungu kwa kila Jambo... Tungekuwa tunafata kanuni hii ya Mungu kuwa twapaswa kushukuru kwa Kila Jambo naamini kuwa Kijana Fredy asingejitoa uhai wake mwenyewe maana angeshukuru na Maisha yakaendelea. Na kingine Mungu anatukumbusha katika Zaburi 113:7-9 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.Hapa Fredy ndio ilikua nafasi yake ya kuwa mnyonge mbele za Mungu na yeye angempandisha kutoka jaani ambapo jaani kwake ni kwenye Mapenzi ya dhati.

Lakini muda mwingine tukumbuke kuwa Unyonge mwingine ni wa kishetani kataa kuwa mnyonge kwa jina la Yesu na uwinuke kutoka mavumbini Zaburi 136:23 Aliye tukumbuka katika unyonge wetu kwa maana fadhili zake ni zamilele, Ninaposema mavumbini nikuwekwa chini katika kudharauliwa huku ukikanyagwa na kila mtu iwe kazini au kwenye biashara. Mungu huwainua wanyonge na kuwaaibisha wenye nguvu.

Kwa Leo tuishie Hapa.

Imeandikwa na Josephat Lukaza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: