Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athumani, Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa jamaa wa marehemu katika mtaa wa kariakoo unguja leo kutoa mkono wa pole akiwa na waandishi wa habari za michezo Zanzibar (ZASWA).

Kwa taarifa za msemaji wa familia, Nurdin Ramadhani amesema mwili wa marehemu tasafirishwa kesho asubuhi na Boti ya Kampuni ya Azam Marine saa moja asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Kijiji kwao Lushoto siku ya Jumanne mchana.

Mwili wa marehemu utawasili jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi ukitokea Zanzibar baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam utasafirishwa kuelekea kijiji kwao Wilaya ya Lushoto Mkoano Tanga kwa ajili ya mazishi.
 Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Ndg Khamis Said akimfariji kaka wa marehemu, Nurdin Ramadhani alipofika katika msiba kutoa pole leo asubuhi.
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar, Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athuman, Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa Kariakoo, Zanzibar leo asubuhi kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar Zaswa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa Kariakoo, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar, Mwinyimvua Mnzuki akizungumza na waandishi wa habari kwa kupokea kwa masikitiko kifo cha mwandishi mwezao mrehemu Amani Athuman kilichotokea leo asubuhi katika hospitali ya Mnazi Mmoja.
Ndugu wa marehemu wakiwa msibari wakisubiri taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.
Wanafamilia wa marehemu Amina Athumani wakiwa katika msiba huo katika mtaa wa Kariakoo, Zanzibar.

Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: