Tuesday, January 10, 2017

MUSEVENI AMTEUA MWANAWE KUWA MSHAURI MKUU UGANDA

Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba na mkewe Charlotte Kutesa Kainerugaba

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemteua mwanawe Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuwa mshauri mkuu wa rais kuhusu operesheni maalum.

Mke wa Museveni, Bi Janet Kataaha Museveni ni Waziri wa Elimu na Michezo, wadhifa ambao alikabidhiwa Juni mwaka jana.

Jenerali Kainerugaba amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi (SFC) chenye jukumu la kutekeleza operesheni maalum za kijeshi.

Kikosi hicho husimamia ulinzi wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali Uganda.

Luteni kanali Don Nabaasa amepandishwa cheo na kuwa kanali na akateuliwa kaimu kamanda wa SFC.

Rais Museveni pia amemteua mkuu mpya wa majeshi, Meja Jenerali David Muhoozi ambaye amepandishwa cheo na kuwa jenerali.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu