Wakiwa na furaha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Limited, Ubwa Ibrahim baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji Kuku kwa wanachama 3000 wa kampuni hiyo kutoka mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma katika hafla iliyofanyika Kijiji cha Miteja, wilayani humo juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka akifungua mlango katika banda la vifaranga vya mbegu vya mradi huo.

Vifaranga vya mbegu ya kuku wa kienyeji vinavyofugwa kisasa.

Mpiga Picha wa Gazeti la Tanzania Daima, Said Powa ambaye aliliwakilisha kundi la Wananchama Wanahabari la Kwanza One akipokea cheti cha usajili kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mjaka wakati wa hafla hiyo.
Kundi la Wanahabari la Kwanza One likishangilia kwa furaha baada ya kukabidhiwa cheti cha kuwa miongoni mwa wanachama watakaoshiriki kwenye mradi huo.

Mbegu za mazao zilizooteshwa kwa ajili ya kulisha kuku.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji Kuu ya Shitindi Poutry Farm, Shitindi (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi, ambapo aliahidi kununua mayai ya wanachama wa ufugaji wa kuku wa Namaingo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo, Ubwa Ibrahim akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Sehemu ya umati uliohudhuria hafla hiyo.

Mjaka akihutubia wakati wa hafla hiyo.

Moja ya mabanda ya kuku yaliyoandaliwa kwa ajili ya ufugaji.

Wanachama wakifurahia baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa Biashara cha Brela.Mwenyekiti wa Namaingo Mkoa wa Ruvuma akipokea cheti cha Brela

Dk. Hassan Kijaki Mtaalalamu wa Mifugo wa Mkoa wa Lindi akielezea kufurahishwa na kitendo cha Namaingo kuwekeza mradi wa kuku mkoani humo.

Mchumi wa Mkoa wa John Mwalongo akihutubia wakati wa hafla hiyo.

Bi Ubwa na Mjaka wakikagua bidhaa mbalimbali za wAJASIRIAMALI ZILIZOFUNGWA KWA NJIA YA KISASA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: