Rais wa Marekani Donald Trump atia saini amri kuu kuweka masharti juu ya wahamiaji wanaoingia nchini humo. Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani zinasema kuwa, Rais Trump ameanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico baada ya kuzuru makao makuu ya wizara ya usalama wa ndani nchini humo.

Aidha, anatarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata visa kwa wageni kutoka maeneo ya Mashariki ya Kati na Afrika ambayo yana Waislamu wengi.

Miongoni mwa nchi zitakazoathiriwa na agizo la Trump ni Syria, Yemen, Iran, Sudan , Somalia na Iraq.

Rais Trump ameandika kwenye Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani. Mwandishi wa BBC David Willis kutoka Washington anasema hatua hiyo huenda ikayaudhi mashirika ya kibinadamu na yale ya kutoa misaada ikizingatiwa mzozo unaoendelea kwa sasa kuhusu hali ya wakimbizi wa Syria.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: