Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan akiwa ameambana na mkewe Mama Emine Erdogan, wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Erdogan atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia leo tarehe 22 Januari, 2017.
RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na mgeni wake RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan mara baada ya kuwasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,kulia ni mke wa Rais wa Uturuki, Mama Emine Erdogan
RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.

Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak. Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: