Mtazania Alphonce Simbu akimalizia mbio za Mumbai Marathon baada ya kuongoza na kwashinda wapinzania wake katika mbio hizo.
Mtazania Alphonce Simbu wa pili kutoka kushoto akiwa na washindi wenzake waliomfuatia mara baada ya kumalizia mbio hizoza Mumbai Marathon akiwa mshindi wa kwanza.
Mtazania Alphonce Simbu akionyesha medali yake ya dhahabu aliyojishindia katika mbio za Mumbai Marathon baada ya kuongoza na kwashinda wapinzania wake katika mbio hizo.
---
Mtazania Alphonce Simbu, ameibuka mshindi wa mashindano ya Mumbai Marathon ya mwaka huu huku akimtimulia vumbi Mkenya Joshua Kipkorir katika kundi la wakimbiaji wa nje. Mtanzania huyo aliongoza huku akifuatiwa na Wakenya 7 na Waethiopia 2 katika 10 bora.

Mashindano hayo yajulikanayo kama Standard Chartered Mumbai Marathon yanafanyika kila Jumapili ya tatu ya mwezi Januari katika jiji la Mumbai nchini India na ni mbio zinazoaminika kuwa kubwa kabisa barani Asia kwa idadi ya washiriki wanaomaliza.

Simbu, ambaye anadhaminiwa na kampuni ya Multichoice Tanzania, aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa 2:09:28 muda ambao ni mzuri sana kwa mbio za aina hiyo. 

Akizungumzia ushindi wake, Simbu amesema kuwa anaamini ushindi huo umesababishwa na maandalizi aliyoyafanya na kwamba udhamini wa kampuni ya Multichoice Tanzania umemsaidia sana kwani imekuwa rahisi yeye kutumia muda mwingi zaidi kwenye mazoezi na maandalizi.

Amesema anauchukulia ushindi huo kama changamoto kwa mashindano mengine makubwa na kwamba huo ni mwanzo tu. Amesisitiza kuwa ushindi huo siyo wake peke yake au Multichoice , bali ni ushindi wa Taifa zima la Tanzania.Kwa upande wake Mkuu wa Mahusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana amesema Multichoice imefurahishwa sana na matokeo hayo na kwamba wataendela kumdhamini Simbu kwa mujibu wa makubaliano yao, ili kuhakikisha anaendelea kufanya vyema na kuliletea taifa sifa kubwa.

“Tulichukua jukumu la kumdhamini simbu katika mazoezi na maandalizi yake kwa kipindi cha mwaka mzima, kwani tunafahamu fika kuwa mazoezi na maandalizi ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika mchezo wowote. Alisema Mshana na kuongeza “dhamira yetu kubwa ni kuinua vipaji na kulirejesha taifa letu kwenye ramani ya dunia katika ulingo wa michezo na burudani”

Katika mbio hizo, waigizaji maarufu wa .Bollywood John Abraham and Neha Dhupia walikuwepo kuleta amsha amsha kwa washiriki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: