Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi juu ya uhakiki wa Tin Namba leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imesema uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi ‘TIN Number’ kwa Mkoa wa Dar es Salaam na umekwisha na uhakiki mwingine utahamia Mikoa mingine.

Akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi ,jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema uhakiki TIN Number muda wake ulikuwa ikiongezeka kutokana na mahitaji.

Kayombo amesema kuwa kwa sasa muda hautaongezwa na wenye Tin number hawatakiwi kutumia mpaka pele watapopata maelezo katika ofisi za TRA ili waweze kuendelea kutumia namba hizo.

 Sehemu baadhi ya wananchi wakiwa katika uhakiki wa TIN namba leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii).
Amesema uhakiki huo ulianza Agasti hadi Oktoba na kuongeza tena muda wa miezi mitatu ambao umeishia leo.

Kayombo amesema kuwa wale ambao wana Tin number na zinadaiwa TRA wanazo na wanatakiwa kulipa kodi zao ambazo wanadaiwa.

Amesema uhakiki wa Number wa unasaidia kupata taarifa za mfanyabiashara kwa kwa namba ya simu, makazi, sehemu anayofanyia kazi pamoja na anuani za mlipa kodi.

‘’Watu wote wenye Tin Number wasizitumie mpaka pele watapokuwa wamepata maelezo juu ya kuzitumia namba hizo za utambulisho wa wafanyabiashara’’ amesema Kayombo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: