Kuna kisa kipo katika Bible cha don mmoja (tajiri) aliyeitwa Nabali. Huyu jamaa alikuwa na status kubwa, mali za kumwaga to the level kwamba alikuwa anaweza kuandaa hafla za hadhi ya kifalme. Challenge ya huyu Nabali ni kwamba hakuwa na akili wala busara. Mke wa "huyu tajiri jinga" aliitwa Abigaili na unaambiwa alikuwa "mwanamke fulani amazing sana", kuanzia sura, akili, heshima, mpaka shepu kiasi kwamba asingeweza kutokea mahali "mwanaume kamili mithili ya Daudi (mfalme) eti usivutiwe nae"!

Daudi akiwa katika mishe mishe za kupindua serikali ya Mfalme Sauli ikatokea yuko eneo fulani mafichoni ambako Nabali alikuwa na ngome yake ya kibiashara. Kiroho safi, Daud na jeshi lake la waasi akaamua kuwalinda wafanyakazi na mali zote za Nabali (of course Daudi alikuwa na uwezo wa kuteka zile mali). Baadae kidogo Daudi akaishiwa vyakula huko mafichoni, so akatuma ujumbe kwenda kwa Nabali kuomba msaada. Hee! Jamaa si akamtolea nje, Daudi! Aisee, unaambiwa Daudi alimaindi sana kiasi kwamba akapanga kwenda kumua kabisa Nabali na familia yote, maana sio kwa kukosa shukrani kule! Mke wa jamaa (I mean Abigaili) akazipata news, ikabidi atoke mkuku kwenda kwa Daudi kuomba msamaha kwa niaba ya mume wake. Daudi akagahairi kutekeleza unyama kwenye ile familia. (1 Samw 25:2-44)

Actually, sijaja kukupa Bible story, ila nimekupa in summary hiki kisa Ili ili nipate "upenyo" wa kuzungumza na wanaume (hasa waliooa), pointi zifuatazo:-

1). Kama kuna janga kubwa katika ndoa nyingi sasa hivi basi ni tabia za wanaume waliooa kutoambatana na Mungu seriously wala kujihusisha na maombi kwa ajili ya ndoa na familia zao. Unajua Bible inasema kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa na tena inasema waume ishini na wake zenu kwa akili. Maarifa ndio akili. Huwezi kuwa na akili za kuishi na mke wako kama haumchi Mungu na kusimama katika maombi "seriously". Kama hauko na Mungu seriously na unaona ndoa inaenda bila shida, I can gurantee you kwamba anguko lako haliko mbali, utalia muda si mrefu!

2). Pointi ya hapo juu unaweza kui-diss may be kwa sababu ni ya kwenye Bible. Enewei, cheki hii:- Kisaikolojia na kiasili, wanawake wote wanavutiwa na wanaume wenye akili. Kama umeoa na hujiongezi kuinoa akili, uwe na uhakika kwamba mkeo unamboa na huenda tayari anavutiwa na wengine wenye akili ama anaelekea kuvutiwa na wengine wenye akili! Unabisha? Ukimfuatilia Abigaili, ukisoma kwa umakini maneno aliyomwambia Daudi wakati anaomba ule msamaha utagundua wazi kabisa kwamba Abigail "alitegeka ile mbaya", mbele ya Daudi. Yaani kimjini-mjini tunasema Abigaili alionesha "kafa kaoza kimapenzi" mbele za Daudi! Usimlaumu Abigaili, unadhani angefanyeje wakati nyumbani ana mume mpumbavu asiejielewa wala kuelewa wajibu wake?

3). Usipokuwa na akili, (trust me a hundred percent) ya kwamba moyo wa mke wako utahama kwako(yaani hautakuwa kwako). Moyo ukihama kuna hatari mbili:- a) mke ataishi akikudharau (as Abigaili alionesha waziwazi kwa maneno) b) Mke atakuwa mchepukaji mzuri licha ya kwamba bado unaishi nae kwenye ndoa. Usibishe! Ukitaka kujua kwamba moyo wa Abigaili ulishahamia kwa mwenye akili Daudi tangu kitambo, ni pale ambapo Nabali alifariki halafu in no time Daudi akaenda kumposa (Abigaili) afu Abigaili akakubali bila hata kuuma vidole wala kuchora miguu chini! It means moyo wa Abigaili ulishamzimikia Daudi "kinoma" since day one, na aliishi ndani ya ndoa huku moyo na hisia zikiwa kwa "mwenye akili Daudi". Si unaona msala huu?

4). Kimsingi mume unatakiwa kuwa na majibu YOTE ya mahitaji ya mke wako(kiakili, kiroho, kimwili, kiushauri na kiupendo). Akikosa(kimojawapo), mara nyingi mkeo atatafuta (for good) alichokikosa kwako kwa mwanaume mwingine. Mke wako anaweza kumuendea mtu mwingine(mostly mwanaume kama wewe), kwa nia nzuri tu, labda ushauri wa mausuala ya kiuchumi. Trust me, the day mkeo anatafuta majibu ya changamoto zake nje ya wewe mumewe, usalama wake unakuwa mikononi mwa yule aliemwendea. Akikutana na "washenzi" its very simple and easy "kumlamba". Omba Mungu akutane na "wastaarabu" ambao wanaweza kumsaidia na kumruhusu aende akiwa "mkavu" kama alivyofanya Daudi kwa Abigaili. You know what? Kwa jinsi Abigaili alivyokuwa kataitiwa, laiti Daudi ange-demand kulala nae siku ile ile on the spot, hakuna namna angechomoa, ukizingatia yeye mwenyewe Abigaili alikuwa kamzimikia Daudi! Licha ya Daudi nae kutegeka kwa Abigaili lakini akaona sio fresh "kutembea" na mke wa mtu, so, akamruhusu aende zake atleast for that day!

KWA HIYO:-

Najua leo nimeongea maneno magumu sana hasa kwenu wanaume mliooa, but naomba tu myachukue hata kama yanachoma. Anaweza asiwepo Shehe, Padri, Pasta wala kitabu cha kukueleza haya, so, usinimaindi kivileee ila nishukuru. Can I tell you one more thing wewe mubaba ulieoa? Hear this:- njia pekee ya kumu-mudu mkeo ni kuishi nae kwa akili. Sio akili za Chemistry ama za kufaulia Computer Science, nooo! Ni akili zinazotokana na maarifa ya Mungu! So, as long as unajifanya uko bize na mishe zako, kiasi kwamba huna mida wa kumtafuta Mungu, Im sorry kukufahamisha kwamba mke atakushinda(na usikute ameshakushinda ila bado hujagundua tu), kama sio openly basi secretly! Nimemaliza! #SmartMind

Credit Albert Nyaluke Sanga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: