Meneja Uhusian Airtel Tanzania Jackson Mmbando akizungumza wakati wa kutangaza wachezaji waliochanguliwa kutokana na michuano ya Airtel Rising Stars na kujiunga na timu za taifa za vijana ikiwemo Serengeti Boys.
Mkurugenzi wa ufundi wa soka la vijana TFF Kim Paulsen akizungumza wakati wa kutangaza wachezaji waliochanguliwa kutokana na michuano ya Airtel Rising Stars na kujiunga na timu za taifa za vijana ikiwemo Serengeti Boys.
---
Baada ya kumalizika kwa kliniki ya wiki moja ya Airtel Rising Stars mwishoni mwa wiki jana, wavulana 16 wamechanguliwa kujiunga na timu ya taifa ya Serengeti Boys huku wasichana watatu wakichanguliwa kujiunga na timu ya taifa ya wanawake - Twiga Stars na wengine 17 kuchagulia kuingia timu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Kilimanjaro Queens.

Akiongea na waandishi wa habari leo kutangaza majina ya wachezaji hao, Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi alisema makocha walikuwa na kibarua kigumu kuchangua wachezaji kwani wachezaji wote walionyesha vipaji vya hali ya juu sana. Madadi alisema kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa michuano ya Airtel Rising Stars ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya, uchanguzi dhidi ya wachezaji ulikuwa wakuridhisha.

Tulikuwa na jumla ya wachezaji 65 kwenye kliniki ya Airtel Rising Stars, wavulana 40 na wasichana 25. Ni kweli kuwa wachezaji wote hawawezi kuchanguliwa kuchezea timu ya taifa, lakini wachezaji ambao wamebaki tutaendelea kuwatumia kwenye michuano mbali mbali ya vijana. Pia wengine watachanguliwa na klabu zetu kuchezea timu zao za vijana. Natoa wito kwa uongozi kuwatumia vizuri vijana hao kwani vipaji wanavyo wanahitaji uzoefu tu, alisema Madadi.

Mimi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, nitahakikisha Shirikisho inaengemea kwenye upande wa kukuza timu na mashindano ya vijana ili kujenga timu bora ya Taifa. Natoa shukrani kwa Airtel katika mchango wake wa kukuza soka la vijana hapa nchini. Nina uhakika Airtel itaendelea na mashindano haya ya Airtel Rising Stars ili kuendelea kuibua vipaji vya vijana wetu, alisema Madadi.

Tuko kwenye harakati za kuhakikisha tunakuwa na timu za kudumu za umri wa chini ya miaka ya 14, 17 na 19. Tukifanya hivyo tutaweza kujenga timu ambayo itafanya vizuri kwenye fainali za michuano ya AFCON ambayo itafanyika hapa Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 2019, aliongeza Madadi.

Akiongea juu ya kuchangua wachezaji, kocha mkuu wa timu ya Serengeti Boys Bakari Shime ambaye alisimamia kliniki hiyo alisema makocha walichangua wachezaji kulingana na mahitaji ya sasa ya timu ya Serengeti Boys. Tuliengemea kwenye wachezaji ambao wanaweza kuelewa na kuendana na mfumo wa mpira wa mashidano na wachezaji wenye uelewa wa haraka. Kama mnavyojua, timu yetu ya Serengeti imecheza mechi nyingi za kimataifa kwenye miaka miwili iliyopita na hivyo kupata uzoefu wa kimataifa. Nia yetu ilikuwa kupata wachezaji wa kuendana na mfumo huo, alisema Shime.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza wachezaji waliochanguliwa kujiunga na timu za taifa. Wachezaji hawa walianza kucheza michuano ya Airtel Rising Stars tangu ngazi ya wilaya. “ Airtel tunayo furaha kuweza kuwafanya wachezaji hawa kutimiza ndoto zao za kucheza mpira wa kulipwa. Kama mnavyojua mpira kwa sasa sio burudani pekee, bali pia ni ajira kwa wachezaji wengi duniani. Ni hamasa kubwa kuona vijana wakianza kujipatia riziki zao kutokana na vipaji vyao vya kucheza mpira wa miguu” alisema Mmbando.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: