Thursday, January 5, 2017

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUMZIKA KAPTENI MHAIKI, SONGEA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakiweka shada la maua katika kaburi la aliye kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali Kapteni Kenan Mhaiki aliyefariki tarehe 31/12/2016 na kuzikwa tarehe 4/1/2017 kijijini kwao Matogoro Mkoani Ruvuma.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za serikali katika misa ya kumuombea marehemu Kapteni Kenan Mhaiki iliyofanyika katika kanisa la Jimbo kuu Katoliki la Songea Parokia ya Mtoto Yesu Matogoro, Songea.
Mjane wa Marehemu Kapteni Kenan Mhaiki akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake
Watoto wa Marehemu Kapteni Kenan Mhaiki wakiweka Mashada ya maua katika kaburi la Baba yao.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Kapteni Kenan Mhaiki wakati wa misa ya kumuombea katika kanisa la Jimbo kuu Katoliki la Songea Parokia ya Mtoto Yesu Matogoro, Songea. Picha na Chris Mfinanga.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu