Friday, February 10, 2017

ASILIMIA 17.89 YA WA WANAFUNZI WAINGIA MITINI KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MKOANI IRINGA
Mkuu wa Iringa Amina Masenza akisalimiana na walimu wa shule ya sekondari Lundamatwe Kilolo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikagua vyumba vya madarasa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Lundamatwe wilaya ya  Kilolo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikagua madaftari ya wanafunzi shule ya sekondari Lundamatwe wilaya ya kilolo wakati wa ziara yake.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikagua idadi ya wanafunzi walioripoti kuanza na kidato cha kwanza shule ya sekondari Lundamatwe Kilolo huku wanafuzi hao wakiwa wamekaa kwa kubanana viti vitatu wakikaa wanafunzi wanne.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah kushoto akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa kikao cha majumuisho wilayani Kilolo
Na matukiodaima blog , Kilolo- Iringa.

SERIKALI ya Mkoa wa Iringa imeagiza wazazi walioshindwa kupeleka Watoto waliofaulu kujiunga na sekondari wasakwe.

Agizo hilo imetolewa leo na mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa vyumba vya madarasa kwenye Shule za sekondari wilaya ya Kilolo.

Alisema kuwa ni wajibu wa watendaji wa vijiji na kata kushirikiana na Walimu wakuu wa Shule pamoja na waratibu elimu kata kujua idadi ya watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuona wameripoti Shule.

"Nawaagiza watendaji wote kufanya msako wa watoto walioshinda kujiunga na elimu ya sekondari"

Alisema mbali ya watoto hao kusakwa pia lazima wazazi wabanwe kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wao wa kupeleka kuwapeleka Shule

Mkuu alisema lengo la serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ni kuona kila mtoto anakwenda Shule na ndiyo sababu ya kufuta ada.

Hivyo alisema kwa mzazi atakayeshindwa kusomesha mtoto anapaswa kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.

Alisema mfano katika Shule ya sekondari Lundamatwe kati ya watoto waliopaswa kujiunga na sekondari hadi sasa ni watoto wanne ndio walichelewa kujiunga ila baada ya wazazi kubanwa Watoto.

Wawili wameripoti na Watoto wawili wanasakwa na kwa wilaya asilimia 17.89 ya Watoto waliochaguliwa kujiunga sekondari hawajaripoti.

"Naagiza hawa Watoto wawili waliokaa nyumbani watafutwe na waletwe Shule kama suala ni umbali wa Shule basi waletwe kuishi hosteli "

Kuhusu maabara mkuu huyo alisema bado kuna changamoto kubwa ya maabara kutokana na wilaya hiyo kugeuza vyumba vya madarasa kuwa maabara hivyo kupelekea upungufu vya vyumba vya madarasa pamoja na maabara zilizo nyingi kuwa chini ya kiwango.

Masenza alimwagiza mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah na uongozi wa halmashauri ya kilolo kufanya jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara borabora

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa kasi ya kuwabana wazazi wasiopeleka Shule Watoto inaendelea na wametoa muda hadi machi wazazi wote kupeleka Watoto wao Shule.

Kwa mujibu wa Afisa Elimu Kilolo Stephen Mrosso jumla ya wanafunzi 3734 ndio walichaguliwa kujiunga na sekondari kati yao wavulana 1658 na wasichana 2076 wanafunzi walioripoti ni 2987 wavulana 1287 na wasichana1693.

Wakati wanafunzi ambao hawajaripoti ni 747 wasichana 383 na wavulana 364 kuwa taarifa zilizopo wanafunzi 82 wakiwemo wavulana 36 na wasichana 46 wamejiunga na Shule nyingine nje ya wilaya ya Kilolo na kufanya jumla ya wanafunzi waliopo Shule kufikia 3069 sawa na asilimia 82.19 hivyo bado asilimia 17.89 kuripoti shule.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu