Tuesday, February 21, 2017

CHAMA CHA WANAWAKE TAWLA CHAKUTANA NA MADIWANI WA WILAYA TATU ZA JIJI LA DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile akizungumza na Waganga Wakuu wa Wilaya, Maafisa Maendeleo wa Jamii, Wanasheria, Madiwani na Maafisa Mipango wa Halmashauri/Wilaya kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar Es Salaam Kinondoni Ilala na Temeke pamoja na Waandishi wa habari waliopata fursa ya kushiriki wakati akifungua semina ya kupata mrejesho wa maazimio kuhusu rasilimali zinazoboresha haki ya afya ya uzazi kwa upande wa mamlaka za Halmashauri ya jiji la Dar Es Salaam; na pia Kupata mrejesho juu ya utekelezwaji wa maazimio yaliyowekwa na kila Halmashauri/Wilaya kufuatia semina shirikishi iliyofanyika mwaka 2016 Mkoani hapa.Semina hiyo imefanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo.
Nancy Richard Mkuu wa Idara ya Huduma za Msaada wa Kisheria TAWLA akizungumza jambo wakati wa semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam anayefuatia kwenye picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile pamoja na washiriki wengine wa semina hiyo.
Nancy Richard Mkuu wa Idara ya Huduma za Msaada wa Kisheria TAWLA akifafanua jambo wakati wa semina hiyo kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile.
Mwanaharakati na Mtetezi wa Haki za wanawake na wanaume Mary Lusimbi ambaye ndiye alikuwa mwezeshaji wa semina hiyo akitoa mada kwa washiriki wakati semina hiyo ilipokuwa ikiendelea.
Bi. Halili Katani Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni akichangia hoja wakati wa semina hiyo kulia ni Balima Omari Afisa Maendeleo ya Jamii Manipaa ya Kinondoni na katikati ni Tausi Kheri Mwanasheria wa Manispaa ya Kinondoni
Baadhi ya washiriki waki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo.
Tausi Kheri Mwanasheria wa Manispaa ya Kinondoni akichangia hoja wakati wa semina hiyo kutoka kulia ni Kheri Missinga Diwani Kata ya Bunju, Balima Omari Afisa Maendeleo ya Jamii Manipaa ya Kinondoni na Kushoto ni Bi. Halili Katani Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile akifafanua mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu