Saturday, February 11, 2017

KONGAMANO KUBWA LA MAOMBI MAALUMU KWA WANAVYUO LAFANYIKA MKOANI SHINYANGA

Leo Jumamosi Februari 11,2017 kumefanyika kongamano kubwa la Maalum la Maombi kwa Wanavyuo mkoani Shinyanga.

Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali mkoani Shinyanga,viongozi wa vyuo na dini,wanakwaya,wanafunzi wa shule za sekondari na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.

Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Kongamano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani Shinyanga limetokea baada ya Mtumishi wa Mungu Happiness Mwaja Kihama kutamani kuwepo kwa kongamano ndipo wanafunzi kwa pamoja wakakubali kuunganisha nguvu hatimaye kufanikisha kufanyika kwa kongamano hilo.

Miongoni mwa malengo ya Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Kumcha Bwana ni Chanzo cha Maarifa –Mithali 1:7”ni kuwaleta pamoja wanafunzi na kuwafanya wafahamiane,kuunganisha nguvu katika kumuomba mungu kwa ajili ya kuendelea ustawi wa kielimu katika mkoa wa Shinyanga.

Pamoja na kuuombea mkoa wa Shinyanga kielimu,kongamano hilo pia lililenga kuwaombea wanafunzi ili mungu awasaidie kufanya vizuri katika masomo yao sambamba na kuwajengea uwezo vijana uwezo wa kumjua mungu na kusababisha hofu ya mungu ndani yao ili kuisadia serikali katika kupunguza vitendo viovu katika jamii.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu