Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatano Februari 15,2017 ameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia miundo mbinu iliyopo katika jimbo hilo.

Siku ya kwanza ya ziara ya mbunge huyo ilikuwa katika kata ya Kolandoto,Ibadakuli,Shinyanga Mjini,Kambarage na Ngokolo.

Mheshimiwa Masele alikuwa ameambatana na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi pamoja na wataalam kutoka idara mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga.

Mheshimiwa Masele ametembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga ambalo lipo kati mto mkubwa maarufu kwa jina la ‘Mto Simba’.

Mbunge huyo pia amejionea jinsi barabara ya kutoka barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza kwenda hospitali ya Kolandoto ilivyokatika na kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Kolandoto.

Ziara ya Mbunge Masele pia ilifika katika masoko makubwa yaliyopo katika jimbo hilo ikiwemo soko la Kambarage lililopo kata ya Kambarage,Nguzo Nane lililopo kata ya Shinyanga mjini,soko kuu la mkoa wa Shinyanga na soko la Mitumba maarufu ‘Ngokolo Mitumbani’ lililopo kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo katika ziara hiyo ametuletea picha 44 za matukio yaliyojiri kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele.
Hapa ni katika Barabara ya Kolandoto- Wami ambayo inatoka katika barabara kuu ya Shinyanga- Mwanza-Kushoto ni Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akimuonesha mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele (wa pili kushoto) jinsi barabara hiyo ilivyomong’onyoka hali inayotishia kukatika kwa barabara hiyo inayoelekea katika hospitali ya Kolandoto.
Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akiendelea kutoa maelezo ingawa hata hivyo mbunge Masele aliahidi kutengenezwa/kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango kwa fedha za mfuko wa jimbo la Shinyanga mjini wakati wanafanya utarabu wa kujenga barabara hiyo katika kiwango cha lami.
Hapa ni katika Ofisi ya CCM Kata ya Kolandoto-Aliyesimama ni Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akizungumza wakati akimkaribisha mheshimiwa Masele aweze kuzungumza na baadhi ya wananchi wa kata hiyo huku akibainisha kuwa ziara hiyo inalenga kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Diwani wa Kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya ambaye pia ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga akielezea changamoto ya gharama kubwa za matibabu katika hospitali ya Kolandoto hali inayosababisha wananchi wa eneo hilo wakose huduma ya afya kama inavyotakiwa matokeo yake kulazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma hiyo katika kituo cha Afya Kambarage au Zahanati ya Galamba.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi wa kata ya Kolandoto ambapo alisema ziara hiyo siyo ya siasa bali ni kiutendaji
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wananchi hao na kuwaeleza namna serikali inavyojitahidi kuhakikisha kuwa kero zao zinamalizika
Hapa ni katika Mto Simba ambapo mradi wa Ujenzi wa Daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga unaendelea.Pichani ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia upande wa pili wa daraja linalojengwa na Mkandarasi M/S Pasons Co.Ltd tangu mwezi Juni mwaka 2016 na unatarajia kukamilika mwezi Machi mwaka 2017.


Ujenzi wa daraja ukiendelea
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishindilia zege kwa kutumia mashine kwenye daraja hilo


Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza kwenye daraja la Galamba ambapo alisema ujenzi huo wa daraja ambalo litaboresha mawasiliano katika kata ya Kolandoto na manispaa ya Shinyanga kwa ujumla ni miongoni mwa ahadi ambazo aliahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.
Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd akielezea mradi huo wa daraja ambapo alisema mpaka sasa ameshakamilisha ujenzi wa vitako vyote vya daraja na ujenzi wa kuta/nguzo zote za daraja na kwamba anaendelea kutengeneza kindanda cha daraja ya upande mmoja na kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 75.
Ujenzi unaendelea
Muonekano wa daraja na eneo ambapo mto Simba unapita
Mheshimiwa Masele akiteta jambo na Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd
Mheshimiwa Masele akizungumza katika shule ya msingi Bugweto na kuwataarifu wanafunzi na walimu wa shule hiyo kuwa ametoa mifuko 100 ya saraji kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo ambayo yamechakaa na hayana sakafu sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Bugweto
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya darasa la saba katika shule ya msingi Bugweto.
Darasa likiwa lina kokoto na vumbi sakafuni

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: