Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Illuminatha Mwenda akisoma taarifa fupi wakati wa kukabidhi mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe,Edwin Mwanzinga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe,Edwin Mwanzinga akimkabidhi Manager wa SACCOS ya ANGLICAN NJOMBE Marco Haule hundi yenye thamani ya Tsh. Million 47,500,000/=
Mwenyekiti wa kikundi cha Ujasiriamali cha Vijana kijulikanacho kama A LUCKY NUMBER GROUP Stanley Mgaya akipokea hundi yenye thamani ya Tsh. Milioni Mbili (2,000,000/=)
Mwakilishi wa kikundi cha Wanawake kijulikanacho kama UJASIRI GROUP akipokea hundi yenye thamani ya Tsh Million tatu (3,000,000/= kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Edwin Mwanzinga.
Wataalamu kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Njombe wanaojihusisha na ufuatiliaji na usimamizi wa mikopo ya Wanawake na Vijana wakifuatilia kwa makini zoezi la utoaji mikopo.
---
HYASINTA KISSIMA- NJOMBE

Katika kutekeleza agizo la Serikali la kuhakikisha kuwa Halmashauri inatenga asilimia 10 za makusanyo yake kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya Vijana wanawake Halmashauri ya Mji Njombe imefanikisha azma ya serikali kwa kutoa mikopo yenye thamani ya Tsh, 106,400,000/= (milioni Mia Moja na sita na laki nne kwa jumla ya vikundi 51 vya wanawake na vijana na Sacccos 8 zilizopo katika Halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Illuminatha Mwenda amesema kuwa fedha hizo zimetokana na uchangiaji wa mapato ya ndani ambapo Halmashauri imechangia Tsh. 56,400,000/=, na Tsh. 50,000,000/= ikiwa ni fedha zilizotokana na marejesho ya vikundi kutokana na mikopo iliyotolewa awali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Edwin Mwanzinga amesema kuwa ni vyema vikundi hivyo vikatumia fedha hizo kulingana na shughuli ambazo wamekuwa wanazifanya ili vikundi hivyo viweze kujiendesha na kufanya marejesho kwa wakati kwani kumekuwa na changamoto nyingi za vikundi kushindwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati na hivyo kusababisha vikundi vingine kushindwa kupata mikopo.

“Napenda nivipongeze vikundi vya wanawake na sitaacha kuvipongeza kwani wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa vinarudisha marejesho kwa wakati na ndio maana ukiangalia katika vikundi tunavyovipatia mikopo leo hii idadi kubwa ni ya vikundi vya wanawake vijana ni vikundi 19 tuu kati ya 51 huu sio upendeleo ni kutokana na kuwa wamekuwa wanaminifu katika kurejesha mikopo. Vikundi vya Vijana wengi mmekuwa sio waaminifu sisi tutakuwa tunaangalia wale wanaoendana na kasi ya urejeshaji mikopo ndio tutawapatia mikopo hivyo nitoe rai kwenu ninyi vijana kuhakikisha kuwa mnakuwa waaminifu katika kurejesha mikopo kwa wakati.”Alisema Mwanzinga.

Aidha, amevitaka vikundi hivyo kuhakikisha wanawapatia elimu watu wanaokwepa kulipa mapato mbalimbali ya Halmashauri na wawe mifano kwa kuonesha kuwa wao ni wanufaika namba moja wa makusanyo yanayofanywa na Halmashauri na waelimishe na kuhamasisha uchangiaji wa mapato kwani kwa kukwepa kulipa mapato hayo ndipo kunaposababisha mikopo kutolewa midogo kwani mikopo inayotolewa inatolewa kulingana na kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.

Katika kipindi cha robo ya kwanza na robo ya pili ya mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya Tsh. Millioni 158,400,000 na imejipanga kuendelea kutoa mikopo zaidi katika robo ya tatu na ya nne kwa kadiri Halmashauri itakavyokusanya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: