Friday, February 3, 2017

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA, JENERALI VENANCE MABEYO

Rais John Pombe Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania akichukua mahala pake jenerali Davis Mwamunyange aliyestaafu.

Taarifa kutoka ikulu iliotumwa katika vyombo vya habari inasema kuwa Luteni huyo sasa amepandishwa cheo na kuwa jenerali kamili.

Wakati huohuo rais amemteua meja jenerali James Mwakibolwa kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi akichukua mahala pake Jenerali Mabeyo.Pia yeye alipandishwa cheo cha luteni jenerali.

Tarehe ya kuapishwa kwa wawili hao itatangazwa baadaye.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu