Monday, February 13, 2017

MSANII TID AKIRI KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

 Msanii wa Kizazi Kipya Khalid Salum Mohamed aka TID, leo amekiri kuwa amekuwa akijihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Akizungumza katika mkutano wa kumkaribisha Kamishna Mteule wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya, Rogers William Sianga jijini Dar es Salaam, Msanii huyo aliwaomba watanzania wote kumsamahe kwa kosa alilolifanya la kutumia madawa.

"Nakiri nilikuwa natumia madawa ya kulevya ila nimeuona mkono wa sheria umeweza kunifungua na kweli sasahivi nipo tayari kuiunga mkono hii kampeni ili kuwaumbua watumiaji na wauzaji ili nchi iwe salama," alisema TID.

Pili alimuomba mama yake mzazi kumsaheme kwa kosa hilo alilolofanya., pia aliipongeza serikali kwa juhudi zake zote za kupambana na madawa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu