Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa kimahakama, Bi Sobha Mohamedi ameibua taflani na kugeuka shujaa mara baada ya kufanikiwa kuelezea tuhuma zake kwa namna alivyodhurumiwa haki zake katika mahakama ya mwanzo mkoani Tanga.

Sobha ambaye alifanikiwa kupenya katikati ya watu na kusogea mbele akiwa na bango ambalo lilikuwa likieleza jinsi alivyodhulumiwa kisha kuzuiwa na walinzi wa Rais lakini Rais Dk John Pombe Magufuli akaamuru asogee mbele asikilizwe.
Mama huyo mara baada ya kufika mbele ya Rais aliweza kueleza kila kitu na mwenendo wa jinsi kesi yake ilivyokwenda na hatimae kupewa hukumu ambayo ilikuwa ya pande mbili ambayo haitoi haki ya moja kwa moja ya kuendelea kuwa mmiliki wa mirathi aliyofungua.

Mara baada ya kujieleza hivyo Rais Magufuli aliagiza mamlaka zote kuhakikisha kuwa mahakama na mamlaka zinazo husika kushughulikia kesi hiyo kuhakikisha kuwa haki inatendeka .

Dk Magufuli ameagiza jeshi la Polisi kumpatia mama huyo ulinzi ili aweze kuishi kwa amani bila kubugudhiwa na mtu yeyote,huku akiendelea kutunza ushahidi wa kesi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza mwananchi, Bi. Sobha Mohamed, aliyejitokeza kueleza kero ya masuala ya mirathi anazozipata katika mahakama mbele yake wakati wa sherehe za Kuzindua Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama Mtaa wa Chimala Ocean road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017
Jaji Kiongozi Mhe Ferdinand Wambali akichukua melezo ya mwananchi, Bi. Sobha Mohamed, aliyejitokeza kueleza kero ya masuala ya mirathi anazozipata katika mahakama mbele yake wakati wa sherehe za Kuzinduzi Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama Mtaa wa Chimala Ocean road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. PICHA NA IKULU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: