Picha : Nikimsaidia mama nitilie wa hapa Mkoani Shinyanga kusukuma Chapati.

Inawezekana ewe Rafiki yangu mpendwa wa FACEBOOK/Blogu wakati huu usomapo ujumbe huu, uko ukitafakari juu ya namna mambo yalivyokwenda ndani ya wiki hii inayomalizikia kwa kuwa imekuwa ni BILA BILA tofauti na taraja la moyo wako.

Kwa WAKINGA kuna msemo usemao :

- Kama pwire pwire ( Kikinga )
- Kama ipo ipo tu ( Kiswahili )

- Uvipulikhela nitokha ( Kikinga )
- Angojaye hachoki (Kiswahili)

- UNGULUVE alumanyile ikhilawo jiane / ijiave (Kikinga)
- MUNGU anaijua kesho yako / yangu (Kiswahili )

Sikia ewe Rafiki yangu mpendwa, haijalishi mazingira yako magumu kiasi gani katika kuielekea ile njozi yako iwe ni AJIRA, MKE, MUME, MTOTO , MASOMO nk

Bado usikate tamaa na usikubali mazingira yakukatishe tamaa, MUNGU wako yu hai hata leo. Weka bidii huku ukimtumainia yeye na kumkumbusha juu ya ahadi zake kwako kila leo.

Ninakuombea wewe au yule unayemjua mwenye uhitaji uwao wa namna yoyote ile MUNGU akafanye njia na kuachilia baraka sambamba na kibali kwako katika kila lililo jema unalolitarajia.

BWANA MUNGU tunakuja mbele zako tukiomba haya kwa ni wewe pekee ndiyo jibu la hitaji la wanao wapendwa hawa. Tunasema asante kwa kuwa tunaamini umesikia maombi yetu na utajibu sawa sawa na kalenda yako.
Amen

@ BAGATECH

Godwin D. Msigwa
Shinyanga
Tanzania
11 Februari 2017
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: