Tumpe Ushirikiano Kamishna Sianga Pamoja na DCEA Katika Kupambana na Madawa ya Kulevya Nchini

Kwa dhati kabisa naomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Chama changu kumtakia kila la kheri Kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), ndugu yangu Rogers Sianga. Nawaomba Watanzania wenzangu wote tumuunge mkono na kumpa ushirikiano Kamishna pamoja na mamlaka anayoiongoza ili kuhakikisha tunalimaliza au hata kulipunguza tatizo hili la madawa ya kulevya.

Ni matumaini yangu na Chama changu kuwa DCEA watafanya kazi yao kwa weledi na uadilifu. Kauli yake kuwa DCEA watatenda haki na kufuata sheria katika kukabiliana na janga hili ili kuhakikisha nguvu kazi ya Taifa hili, hasa vijana, hawaathiri zaidi ni ya kutia moyo mno.

Mola amtangulie katika mapambano haya.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Dar es salaam
Februari 13, 2017
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: