Saturday, February 11, 2017

UONGOZI WA SHULE YA SUN ACADEMY IRINGA WAMPONGEZA RAIS DKT. MAGUFULI KWA KUPAMBANA NA UFISADI NA VITA YA DAWA ZA KULEVYA


Mkurugenzi wa shule ya Sun Academi Iringa Chengula Nguvu akitoa pongezi zake kwa Rais Dkt. John Magufuli dhidi ya vita ya dawa za kulevya leo

Mkurugenzi wa shule ya Sun Academi Chengula Nguvu kushoto akimkabidhi zawadi mwalimu mkuu wa shule hiyo James Mwakamele wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa darasa la tano na walimu kwa kuiwezesha shule hiyo kushika nafasi ya pili kiwilaya mtihani wa taifa wa darasa la nne mwaka jana.

Mkurugenzi huyo akikabidhi zawadi kwa walimu.Timu nzima ya walimu wa Sun Academi.

Mmoja kati ya wazazi akimpongeza mtoto wake
Mkurugenzi wa Sun Academi Iringa akimwamasisha mwanafunzi kusoma zaidI.

Mmoja kati ya wazazi akitoa ufafanuzi wa zawadi alizojitolea kwa ajili ya wanafunzi

Na MATUKIODAIMABLOG

UONGOZI wa shule ya Sun Academy Iringa umepongeza kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli katika kupambana na vitendo vya ufisadi ,rushwa na dawa za kulevya kuwa vita hiyo imerejesha heshima ya Taifa.

Akitoa pongezi hizo wakati wa hafala ya kuwapongeza wanafunzi wanafunzi 35 wa darasa la tano ambao walifanya vizuri  katika mitihani ya Taifa ya darasa la nne mwaka jana na kuifanya
shule hiyo kushika nafasi ya pili kwa wilaya ya Iringa kuwa Rais anapaswa kumpongeza Rais Dkt. Magufuli na serikali yake kwani kazi anayoifanya imeleta heshima kubwa kwa taifa .

Bw. Nguvu alisema kwa upande wa ufisadi na Rushwa hivi sasa watanzania wote wameunganishwa pamoja kwa aliye nacho na asiyenancho wapo sawa tofauti na zamani ambapo kulikuwa na matabaka kati ya wenye nacho ambao wanapata kwa njia zisizo sahihi na masikini .

Kwani alisema kubana minya ya ufisadi na rushwa hivi sasa kila mtanzania anaishi kwa heshima kubwa na kila mmoja anatafuta pesa ya haki na sio pesa za ufisadi na rushwa .

Kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya alisema matunda ya vita hiyo yanaonekana kwa kila mmoja tena ndani ya kipindi kifupi sana na kuwa wanaobeza jitihada hizo hawajakumbwa na madhara ya dawa hizo za kulevya.

Alisema iwapo ungeshuhudia kuona vijana wanavyo haribika kwa dawa hizo za kulevya na jinsi ambavyo Taifa linavyopoteza nguvu kazi hiyo basi kusingekuwa na mtanzania kusikika akibeza jitihada hizo.

Hivyo pamoja na kumpongeza Rais Dkt Magufuli kwa kazi hiyo bado alimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na wakuu wote wa mikoa pamoja na jeshi la polisi kwa kuendelea na mapambano hayo dhidi ya dawa za kulevya . UONGOZI wa shule ya Sun Academi  Iringa umewahakikishia wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule  hiyo kuendelea kuwa na imani kubwa ya watoto wao kufaulu mtihani wa darasa la saba pia kuendelea kufanya vizuri katika mitihani mbali mbali ya kitaifa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu