Friday, February 24, 2017

WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE YA SEKONDARI ILULA WILAYA YA KILOLO WACHANGIA UKARABATI WA SHULE

Wawakilishi wa wanafunzi waliosoma shule ya sekondari Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mwalimu Nguvu Chengula kushoto na mchungaji Yekonia Koko wakimkabidhi fedha kiasi cha Tsh milioni 1.3 mkuu wa shule ya sekondari Ilula mwalimu Vincent Shauri (katikati) kulia ni makamu mkuu wa shule hiyo Joachim Mlay
Mkuu wa shule ya Sekondari Ilula katikati akiwaonyesha choo cha kisasa kinachojengwa shuleni hapo kwa ajili ya matumizi ya walimu
Mkuu wa shule ya Sekondari Ilula Vicent Shauri kulia akionyesha choo hicho
Hiki ndicho choo cha walimu kinachojengwa shule ya sekondari Ilula.
Mkuu wa shule ya sekondari Ilula akionyesha nguzo za umeme.
Bweni lililoezuliwa na kimbunga likiwa bado kuezekwa.Na MatukiodaimaBlog

WANAFUNZI waliosoma shule ya sekondari Ilula wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wametoa msaada wa fedha kiasi cha Tsh milioni 1.3 kwa ajili ya kuchangia ukarabati wa shule hiyo baada ya kukumbwa na maafa ya kuezuliwa na kimbuka vyumba vya madarasa na bweni la wanafunzi.

Wakikabidhi maasada huo mchungaji Yekonia Koko na Mwalimu Nguvu Chengula jana kwa niaba ya umoja wa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo walisema kuwa wameguswa na changamoto mbali mbali zilizopo katika shule hiyo hasa baada ya kupatwa na maafa ya vyumba vya madarasa na bweni kuezuliwa na kimbunga na kupelekea wanafunzi kuendelea kulala darasani kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Hivyo walisema kupitia umoja wao wanafunzi waliosoma katika shule hiyo wamelazimika kuchangishana fedha ili kusaidia uboreshaji wa shule hiyo kama sehemu ya mchango wao kwa shule hiyo pia njia moja wapo ya uhamasishaji wa wananchi kuendelea kuchangia maendeleo ya elimu badala ya kuiachia serikali.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu