Wednesday, February 8, 2017

WATUHUMIWA WENGINE 65 WA MADAWA YA KULEVYA WATAJWA, WAMO MCHUNGAJI GWAJIMA, YUSUF MANJI, IDDI AZZAN, FREEMAN MBOWE

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja watuhumiwa 65 wa Dawa  za Kulevya,katika majia hayo ametajwa Freeman Mbowe, Mchungaji  Gwajima,Yusuf Manji, Idd Azzan.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake mapema leo jijini Dar, Mhe. Makonda  ameingia katika awamu ya pili ya kutaja majina hayo na kuyaweka hadharani, huku akieleza kuwa watuhumiwa hao watatakiwa kufika kituo cha polisi kati  siku ya Ijumaa, saa tano asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Katika hatua nyingine Mhe. Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha  Radio ya EFM,ajulikanae kwa jina la Francis Ciza, almaarufu kwa jina la Dj Majay. "tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata Wahusika weote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kwa mahojiano zaidi;" alisema Makonda.

Watuhumiwa wa sakala hilo la Dawa za kulevya.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu