Friday, February 10, 2017

WIZARA YA FEDHA YAMLIPA MKANDARASI ANAYEJENGA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (TERMINAL 3) FEDHA ZOTE ANAZODAI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (pichani) akizungumza na wanahabari kuhusu Wizara yake ilivyotekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufu kuhusu kumlipa Mkandarasi anayejenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Doto James, Wizara ya Fedha na Mipango imemlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Kampuni ya BAM International kiasi cha Euro Milioni 9.5 sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 22 za Kitanzania mara baada ya kuhakiki madai hayo.

Katika Hatua nyingine Wizara ya Fedha inaandaa Malipo ya awali (Advance Payment) kiasi cha Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Kutumia Umeme na Mafuta(Standard Gauge) katika awamu ya kwanza itakayoanzia kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu yake ya kwanza ya Ujenzi huo. Picha na Mpiga picha Wetu

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu