Gari aina ya Mark II Grand yenye namba za usajili T145AMZ likiwa limeivaa daladala lenye namba za usajili T992DGZ lililokuwa limepaki kituoni KIMARA -SUKA jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa wapo eneo la tukio ilionyesha dereva wa gari hilo dogo alikuwa amelewa na ndipo aliposhindwa kukamata breki na kujikuta uvunguni kwa daladala hilo. Tukio hilo lililotokea majira ya saa 4 usiku wa tarehe 17.03.2017
Vijana wakijaribu kuiba katika gari ndogo iliyokuwa imepata ajali eneo la Kimara Suka jijini Dar es Salaam.
Vijana ambao walivamia gari ndogo na kuanza kuiba wakishangaa kuona kamera ya Kajunason Blog imetinga eneo hilo na ndipo walipoungana na mwenye gari kumfanyia fujo na kumpiga kwa kumshambulia mwandishi wa habari Cathbert Angelo Kajuna aliyekuwa eneo la tukio. Kwa msaada wa wasamalia wema waliweza kumnasua mwandishi huyo na kuweza kumshika kijana aliyekuwa mmiliki wa gari ndogo ambaye ndiye alitoa amri ya kumshambulia mwandishi wa habari.

Kijana aliyemshambulia mwandishi wa habari Cathbert Angelo Kajuna amekatwa na kufunguliwa jarada la KMR/RB/3987/2017 na mpaka sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Mbezi kwa Yusuph.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: