Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, akiwasilisha mada juu ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania, wakati wa semina ya Wiki moja kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, tawi la Zanzibar, leo Machi 28, 2017.
Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT), Bi. Zalia Mbeo, akifafanua baadhi ya hoja zilizoulizwa na waandishi wa habari kuhusu mada ya Sera ya Fedha.
Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina akizunhuzma mwanzoni mwa warsha hiyo
Mwandishi wa habari za Biashara na Uchumi wa Azam TV, Bi. Rahma Salum akizungumza
Bw.Genes Kimari, (kushoto), na Bw. Mohammed Kailwa wote kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha -BoT
Meneja Masoko ya Ndani Kurugenzi ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw.Reverian Mbeo, akizunhuzma wakati akiwasilisha mada juu ya Majukumu ya Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Utekelezaji wa sera ya fedha wa Benki
Kutoka kulia, Meneja wa Fedha na Utawala, Bodi ya Bima ya Amana ya BoT, Bw. Richard Malisa, Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Zalia Mbeo, Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, na Bw.Mohammed Kailwa kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, BoT.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUMUKO wa bei utokanao na ongezeko la Fedha ni hatari sana katika uchumi wa nchi, Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, ameiambia semina ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kutoka vyombo mbalimbali vya habari leo Machi 28, 2017.

Semina hiyo ya wiki moja inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar, ina lengo la kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusu namna bora ya uandishi w ahabari za uchumi na fedha.

Chini ya Sera ya Fedha, (Monetary Policy), Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kama mtengeneza fedha (mchapishaji), inaweza kudhibiti mfumuko wa bei utokanao na ujazi wa fedha kutokana na viashiria vya uwezo wa uzalishaji katika taifa unapopungua au kuonegzeka. Sera ya fedha maana yake ni pale Benki Kuu inapoamua kuongeza fedha kwenye mzunguko au kupunguza na hii itategemea sana na uzalishaji bidhaa, alifafanua Lusajo.

“Inapogundulika kuwa kiwango cha fedha ni kikubwa kwenye mzunguko kuliko uzalishaji BoT kazi yake hapa ni kupunguza fedha kwenye mzunguko na hii sio kwa eneo fulani tu la nchi bali ni nchi nzima ambako fedha ya Tanzania inatumika.” Alisema Mchumi huyo.

Akifafanua zaidi kuhusu namna BoT inavyoshughulikia ujazi wa fedha au kupunguza, Lusajo alisema njia pkee inayotumika ni kupitia mabenki ya biashara.

“Kama mjuavyo bei ya Mafuta inadhibitiwa na soko la Dunia, na hata mfumuko wa bei za vyakula unategemea na tabia nchi kama ukame unaopelekea upungufu wa chakula, hapa BoT inachofanya ni kutoa usahuri kwa Serikali ili kupitia vyombo vyake ikiwemo vile vya kodi kufanyia kazi hali hiyo.” Alifafanua Mchumi huyo Mwandamizi wa BoT.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: