Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule katika viwanja vya Ngarenaro Jijini Arusha.
Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema, wakwanza kulia ni mbunge wa Simanjiro James OLemilya akifuatiwa na aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro, akifuatiwa na Wema Sepetu,na wakwanza kulia ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha Derick Magoma.
Mbunge Lema akiwa na Wema Sepetu akisaliamia wananchi wa jiji la Arusha.
Mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano jijini Arusha.

Na Vero Ignatus, Arusha.

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoika rumande
alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne.

Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo
tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.

Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha
halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia, sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.

Ameataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: