Kama una date na binti wa umri wa kuanzia miaka ​23​ na kuendelea na hauna mpango wa kumuoa fanya jambo la ​kiungwanana​ kumuambia ukweli.

Sikuambii umwambie kuwa humtaki na hutaki kuoa bali mwambie kuwa wewe si muoaji na unaona kama utampotezea muda wake bure na kuja kumuumiza.

Ongea kiungwana na ikishindikana muache hata kibabe. Hii ni kwasababu mwanamke ​anawekeza vitu vingi katika mahusiano, anawekeza akili yake, mali zake, hisia na kubwa kabisa anawekeza umri wake katika mahusiano​

Unampunguzia uwezekano wa kukutana na mtu sahihi kwa kuendelea kumdanganya. ​Kwa Mwanamke, Age is not just a Number Age is Everything.​

Wakati ukimuacha wewe utatafuta Binti mdogo zadi yake, yeye atalazimika kutafuta kijana mwenye Umri Mkubwa zaidi yake. Ndiyo ilivyo sote Wanaume na Wanawake huangalia ​Umri​ katika Mahusiano.

Ukimchezea na kumuacha akiwa katika umri wa miaka 30, inamaana atafute kijana mwenye umri kuanzia Miaka 32 ambaye bado ni Single. Wako wachache sana wa namna hiyo, sisemi kua hawezi kupata, hapana nasema utampa wakati mgumu na Uhuru wa Kuchagua.

Kuna Umri ambao Mabinti wengi huamua Kuolewa tu, si kwasababu ya Mapenzi bali kwakua hawana namna wanaona kusubiri mtu sahihi watapishana na ​Kalenda.​

Badilika, haikufanyi Mwanaume zaidi kwa kumpotezea Binti wa watu miaka mitano halafu unamuambia ​wewe si Type yangu​ Fanya jambo la Kiungwana na Malizaneni Mapema. Lakini najua kuna Mabinti ambao hawasikii wakiambiwa kuwa mambo yameisha, Mlazimishe asikie na Usimtumie na Kumuumiza kwakua anakupenda.

Women have many possibilities from 12 to 24,but from 25 and above,the graph starts to fall down whether they like it or not, Dear, Women, Men love by reasons #
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: