Mhe. Abbas Mtemvu akisalimiana na baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, alipofika kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba kufungua mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maofisa wa Benki ya Kiislamu ya Amana, wakimpokea mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa wanachama wa Vicoba wa Wilaya ya Temeke na benki hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (wa tatu kushoto), alipofika ukumbini hapo, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakiwa kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba katika mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakiwa kwenye ukumbi wa PTA, katika mkutano wao huo na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wakiwa katika mkutano huo, ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mlezi wa Vicoba, wilayani Temeke, mke wa Mbunge mstaafu wa Temeke, Abbas Mtemvu, Mama Mariam Mtemvu, akiwasalimia wanachama wa vikundi mbalimbali vya vicoba, wakati wa mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, mwishoni mwa wiki.
Mwanachama wa Vicoba, wilayani Temeke, Blandina Makange akisoma risala ya wajasiriamali hao, wakati wa ufunguzi wa mkutano wao huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkurugenzi wa Benki ya Kiislamu ya Amana, Muhidin Ally akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, katika mkutano huo. Katikati ni mgeni rasmi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki hiyo, Munir Rajab.
Mkuu wa Masoko wa benki ya Amana, Dassu Mussa, akizungumza na wanachama wa Vicoba, wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu benki hiyo kwa wajasiriamali hao.
Mjasirimali Elina Amani Ngogo, akiuliza swali kuhusu ukopeshwaji wa viwanja vya makazi unaofanywa na benki ya Amana kwa wateja wake, wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka, akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakati wa ufunguzi, wa mkutano wao, ukumbi wa PTA, Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki ya Amana, Munir Rajab na wa kwanza ni Mkuu wa Masoko wa benki hiyo, Dassu Mussa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: