Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na kushikiliwa na maafisa wa polisi nchini, kuhusiana na wimbo wake wenye jina la "Wapo", ameachiliwa huru mchana wa leo.

Nay wa Mitego ameachiliwa huru kufuatia uamuzi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kupokea ushauri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Hata hivyo Waziri Mwakyembe alimtaka Nay wa Mitego auboreshe zaidi wimbo wake.

Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: