Mwezeshaji wa mafunzo hayo Nyanjura Kalindo akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kijinsia
Mwandishi wa habari gazeti la Nipashe Marco Maduhu akichangia mada wakati wa semina/mafunzo hayo.Kulia kwake ni wanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia kutoka kata ya Mwadui-Luhumbo wilayani Kishapu wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha akiwasisitiza waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu watu wasio na sauti katika jamii
Mwandishi wa habari wa radio Free Africa Malaki Philipo (kulia) na Steve Kanyefu kutoka Radio Faraja fm stereo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na mwezeshaji Rasel Madaha
Mafunzo yanaendelea.Kulia ni mwanaharakati wa masuala ya jinsia kutoka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Kasigwa Adram,katikati ni mwandishi wa habari Sam Bahari akifuatiwa na Charles Jilala ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka wilayani Kishapu
Katikati ni mwandishi wa habari wa DW,Veronica Natalis akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.Wa kwanza kushoto ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Elizabeth Joseph kutoka wilayani Kishapu
Mwandishi wa habari wa gazeti la Jamboleo Stephen Kidoyayi akichangia mada ukumbini.Kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja,bi Moshi Ndugulile
---
Mtandao wa Jinsia (Tanzania Gender Network Programme- TGNP) umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga nakwa ajili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili (Machi 2 na Machi 3 mwaka 2017 katika ukumbi wa Vijana Center katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga pia yamewakutanisha waandishi hao wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa vilivyopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni mwezeshaji Bi Nyanjura Kalindo alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya kijinsia na kuwakutanisha na wanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ili kuongeza nguvu ya pamoja.

“Vipaumbele vya TGNP ni vitano ambavyo ni afya,elimu,kilimo,uziduzi na maji hivyo kwa kuwapatia mafunzo waandishi wa habari tunaamini kabisa itaongeza chachu kuandika habari kwa usahihi zaidi kuhusu masuala ya kijinsia”,alieleza Kalindo.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bwana Rasel Madaha aliwaomba waandishi wa habari kufika katika maeneo ya pembezoni kwani vitendo vya ukatili wa kijinsia yapo na hayaandikwi hali inayosababisha vitendo hivyo kuendelea kujitokeza na kuwafanya baadhi ya watu kuendelea kunyanyasika.
Picha ya pamoja baada ya mafunzo
Picha ya pamojaPicha ya pamoja ,wawezashaji wa mafunzo hayo,Rasel Madaha (kushoto) na Nyanjura Kalindo na Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC).

Picha na Frank Mshana,Stephen Wang'anyi na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: