Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego na wimbo wake kuruhusiwa kupigwa katika vyombo vyote vya redio na televisheni.

Wimbo huo unaojulikana kwa jina la Wapo ulikuwa umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema na leo na yeye mwenyewe kukamatwa akiwa mkoani Morogoro alipoenda kikazi.

Akizungumza na waandishi wa habari mchana huu mjini Dodoma wakati akitoa taarifa hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe amesema uamuzi wa kuruhusiwa kupigwa kwa wimbo umetoka kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli baada ya kupokea ujumbe wa kumtaka hauruhusu wimbo wa msanii huyo kupigwa katika vyombo vyote.

"Wimbo unaozungumziwa Rais Magufuli anaupenda, ameomba aachiwe huru na aendelee na kazi zake, ila anaweza uboresha zaidi wimbo wake huo kwa kuongeza vitu zaidi, kama wakwepa kodi, watumia dawa za kulevya nk". alisema Dkt. Mwakyembe.

Mwakyembe alisema kuwa Rais amefurahishwa na wimbo wa msanii na kumshauri kama inawezekana aendelee kuwataja watu wengine kama vile wauza unga, wakwepa kodi, wabwia unga,wezi na wengine wasio na maadili mema katika jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: