Rais wa Chemba ya Biashara, viwanda na kilimo, Ndibalema Mayanja, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa Mikoa ya Mwanza na Kagera kuchangamkia soko la awali la hisa za TCCIA Investment PLC.
Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa mikoa hiyo bwana Mayanja alisema “TCCIA Investment PLC ni kampuni ya uwekezaji wa pamoja, imara na inafanya vizuri sana kwani tangu ianzishwe mwaka 2005 ikiwa na mtaji wa shilingi Bilion 1.97 imeweza kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6 na imekuwa ikilipa gawiwo kwa wanahisa wake. Hii ni fursa muhimu na adhimu muitumie kabla ya tar 14 mwezi huu March. “ alisema Mayanga.
Rais huyo wa Chemba akiwa ziarani mkoani Mwanza na Kagera pia alifanya kazi ya kujenga uhai wa chemba kwa kukutana na viongozi mbalimbali katika mikoa hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: