*Serikali yakuta hakuna uzalishaji wowote unaendelea

Kampuni ya TDL maarufu konyagi imesitisha utengenezaji za pombe kwa kutumia vifungashio vya plastiki kwa mujibu wa agizo la serikali ambapo mwisho wa kusambaza pombe hizo ulikuwa jana.

Maofisa kutoka Mamlaka ya kusimamia vyakula na Madawa (TFDA), NEMC, TBS na Jeshi la Polisi wamefika kiwandani leo na kukuta hakuna uzalishaji wa vinywaji hivyo unaoendelea kama ambavyo kuna taarifa za kupotosha kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa TDL imekaidi agizo la serikali na imekutwa ikiendelea kufanya uzalishaji kwa kutumia vifungashio vilivyoipigwa marufuku na serikali.

TDL siku zote imekuwa ikiendesha shughuli zake za kibiashara kwa kufuata miongozo na sheria za serikali kupitia taasisi mbalimbali hiyo haiwezi kukaidi na kuendelea na uzalishaji wa kutumia vifungashio vya plastiki wakati vimepigwa marufuku bali inajipanga kutumia teknolojia za kutumia vifungashio vilivyotengenezwa kwa malighafi ya kioo ambavyo vina ubora wa hali ya juu na salama kwa kuwa sio rahisi kuviigiza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: