Ni siku ya furaha kwangu japo ndiyo inachechemea kuisha lakini pia niseme neno tu kwani ukifika wakati kama huu nakuwa naduwaa kwa muda mrefukidogo na sababu ipo tu. Ni siku ya furaha kwani inanikumbusha kuwa mimi si kitu kama asingekuwepo MWANAMKE (yaani mama). Wewe mwanamke uitwaye KASILIDA huko uliko tambua kuwa nakuombea na nina kukumbuka kila wakati. Mama nakupa heshima zote kwani ulikuwa na uwezo wa kutonizaa, ungeweza kunitoa nikiwa bado mimba changa, ulikuwa na kila sababu ya kufanya mimi nisizaliwe lakini mama yangu hata hukuwaza hayo ndo kwanza uliona umebahatika kunipata mimi. Umenizaa na sasa nimekuwa mtu mzima. Ni UPENDO ulioje kwa mwanamke kama huyu. Lakini mama uliondoka duniani ukaniacha nina miaka sita (6) tu hivyo hata sura yako mama siikumbuki vizuri. Nakumbuka usiku mmoja nikiwa nimelala mikononi mwako nyumba yetu ilivamiwa na majambazi ulinificha uvunguni na ukatoka nje wewe ili tu mimi nipone. Na ni kweli leo haupo duniani. Sina zawadi zaidi ya kusema ASANTE SANA MAMA YANGU KWA KUKUBALI NIKUTESE WEWE NIKIWA TUMBONI MWAKO LAKINI UKANIZAA NIKIWA MZIMA.

Mama hukuwahi nionyesha hata mjomba wala mama mdogo. Nilipokuwa ninakuita mama, mama, mama... ulinijibu kwa kunionyesha kuwa ninao mama wengi lakini zaidi uliniambia nimpende na kumuheshimu mwanamke. Leo hii nayakumbuka maneno yako ni kweli haupo lakini ninao mama zangu na nina wapenda ila ukweli ni kwamba mama haupo tena nakukumbuka sana japo najua huko ulipo unaniombea.

Nachukua nafasi hii kuwambia ndugu zangu ambao mama bado wana uzima tafadhali shirikiana nami kumpongeza mama yako popote pale alipo. Nikweli leo wewe ni msomi, unacheo, una nguvu, una sura nzuri lakini kamwe usimfungie mlango mama yako. Mama amebeba mengi sana ambayo hata akikwambia huwezi elewa kabisa na kamwe hathubutu kusema.

Niwasihi dada zangu msitoe mimba kwani leo hii wote tumefanyika baraka kwa familia zetu na Taifa letu kwasababu tu kuna mwanamke aliacha raha zote kwa miezi 9 na kukubali kukuleta wewe duniani.

MWANAMKE NITAKUHESHIMU DAIMA.
Happy Women's Day
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: