Sunday, March 19, 2017

UKARABATI WA BARABARA YA SIMU 2000 JIJINI DAR

Trekta ambalo linafanya kazi ya kukarabari barabara ya Simu 2000
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua barabara ya simu 2000 ambayo ipo kwenye matengenezo ya dharura
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielekeza jambo kuhusu ukarabati wa barabara hiyo, Wengine ni Meneja wa stendi ya Simu 2000 Bakari Shehoza na Injinia wa Ujenzi katika Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga.
Barabara inayofanyiwa maerekebisho.

Na Mathias Canal, Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo leo (Machi 19, 2017) amezuru na kufanya ukaguzi wa barabara ambayo ipo kwenye matengenezo ya dharura.

Barabara hiyo ambayo ni kiungo kati ya wananchi waendao Sinza, Mpaka Mwenge na Posta hadi Kariakoo sawia na Tegeta hadi Bagamoyo Pwani na Wengine kuelekea Ubungo hadi Morogoro ijulikanayo kama simu 2000 iliyopo katika Kata ya Sinza Manispaa ya Ubungo imeanza kutengamaa kwa gari kupita pasipo wasiwasi zaidi ya ilivyokuwa awali.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu