Mmarekani mmoja aliingia kwenye restaurant huko London, ile kuingia tu aligundua kulikuwa na kijana mmjo wa ki-Africa mwenye umri wa kama miaka 28 akiwa amekaa kwenye kona

Yule mmarekani alikwenda mpaka kaunta akatoa kitita cha pesa na kumrushia muhudumu kisha kwa sauti kubwa akasema "muhudumu! namnunulia chakura kila mmoja aliemo humu ndani isipokuwa yule mwafrica pale konani",

Muhudumu alikusanya pesa na kuanza kugawa chakula cha bure kwa kila mtu aliyekuwemo ndani ya restaurant hiyo isipokuwa yule kijana wa kiafrica,

Yule kijana hakukasilika badala yake alimtazama yule mmarekani kisha kwa sauti kubwa akasema "ASANTE SANA"

Yule mmarekani bila kujali kwa mara nyingine tena alivuta kitita cha pesa na kumtupia muhudumu kisha akapayuka "sasahivi nitamnunulia chupa ya wine na nyongeza ya chakula kila mtu aliyemo humu ndani isipokuwa yule mpuuzi aliyekaa pale kwenye kona.

Muhudumu kwa mara nyingine alikusanya ile pesa na kuanza kugawa chakula cha bure na wine kwa kila mtu aliyekuwemo mle ndani isipokuwa yule mwafrica,

Baada ya muhudumu kukamilisha kuwahudumia kwa chakula na vinywaji yule kijana wa kiafrica alimtazama mmarekani kisha akatabasam na kusema kwa mara nyingine "ASANTE SANA"

Hii ilimshangaza yule mmarekani na kuamua kumuuliza muhudumu "hivi yule kijana ana matatizo gani mbona nimenunua chakula na vinywaji kwa kila mtu aliyemo humu ndani isipokuwa yeye lakin hajachukia badala yake amekaa pale anatabasamu na kunishukuru eti "Asante sana!! Au ni chizi?

Muhudumu alitabasamu kisha akasema "hapana siyo chizi, bali yeye ndiye mmiliki wa hii restaurant hivyo anakushukuru kwa kuwa ww ni mteja mzuri"

Kwa uweza wa Mungu maadui zako bila wao wenyewe kujua wakaone kama wanakuangamiza na wakakufanyie mambo mengi ya kukunufaisha na kukuinua ktk maisha yako.
Kama unaamini sema AMEN.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: