Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula katikati akikata utepe wakati wa kuzindua manara wa mawasiliano wa mwakashahala ulipo kijiji cha Ngukumo kata ya Nkiniziwa Wilayani Nzega ambapo pamoja na mnaro huu Airtel imewasha minara mingine mitatu ya mawasiliano katika kata za Kahamanhalanga , Songambele na Itumba na kuwawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kupata huduma za mawasiliano mkoani Tabora. wakishuhudia wapili kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel Tabora, Fidelis Lugangila akiwa pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji cha Ngukumo
---
Wakulima na wafugaji wa kijiji cha Ngukumo kata ya Nkiniziwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wameipongeza Airtel kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya uhakika na kuwawezesha kuangalia bei za bidhaa na kutafuta masoko kupitia simu zao za mkonon

Hayo yalisemwa na wakazi wa kijiji cha Ngukumo wakati wa uzinduzi huduma za mawasiliano utakaowawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kutoka katika vijiji 6 kupata huduma za mawasiliano baada ya Airtel kuwasha minara ya mawasiliano katika maeneo ya Mwakashahalala Kahamanhalanga, Songambele Itumba mkoani hapo

"Tumekuwa tukipata changamoto nyingi sana ikiwemo mawasiiano hafifu ambapo ilibidi kusafiri umbali mrefu kupata huduma za mawasiliano, Tunaishukur kampuni ya Airtel kwa kuona ni vyema kutufikishia huduma za mawasiliano hapa na kutuunganisha na ndugu jamaa na wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi alisema mkazi wa kata ya Nkiniziwa, John.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula alitambua na kupongeza juhudi zinazo fanya na Airtel katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kwa wote kufatia mchango wake muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kusema ni muhimu kuwa na mawasilino bora kwani kichocheo kikubwa katika kuboresha maisha ya watanzania na kurahisisha shughuli zao za kijamaa na kiuchumi.

“Naamini mawasialiano haya yataweesha biashara katika wilaya hii kukua, na wakulima watanufaika na huduma mbalimbali za simu zitakazowawezesha kutafuta masoko ya bidhaa zao, kuangalia bei ya mazao, lakini pia watatumia huduma ya Airtel Money kwaajili ya kufanya malipo na manunuzi kwa njia ya simu. Nawaasa wakazi wa wilaya ya Nzega kutumia mawasiliano haya vyema na kuboresha maisha yao” aliongeza Ngupula.

Kwa upande wake Meneja wa Airtel mkoa wa Tabora, Phidelis Lugangila alisema “Airtel imejipanga kutoa huduma bora na za uhakika na kuwaomba wakazi wa kijiji cha Ngukumo na vijiji vya jirani kutumia huduma na bidhaa za Airtel kupata kipato kupitia huduma zetu kama vile Airtel Money kwa kuwa mawakala na kupata kamisheni kila mwezi na vilevile kutengeneza ajira kwa vijana wengi.

Wakazi wa mwashala wanajishughulisha zaidi na kilimo cha mahindi, pamba ,Karanga na Mpunga pamoja na ufugaji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: