Meneja wa DAWASCO Mkoa wa Ilala, Ndugu Christian Kaoneka akiongea na waandishi wa habari juu Mpango mahususi Kwa watumiaji wa huduma ya Maji ya visima kujiunga rasmi na mfumo wa Majisafi kutoka DAWASCO. 
---


Wamiliki na watumiaji wa Maji ya visima hususani wakazi wa ilala jijini Dar es salaam wametakiwa kujitokeza ili kuunganishiwa huduma ya Majisafi yanayotolewa na shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) ili kuondokana na hujuma inayofanywa na wamiliki wachache wa visima binafsi vya Maji.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Dawasco Mkoa wa Ilala, Christian Kaoneka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mpango wa kuunganishia wamiliki wa visima katika mfumo rasmi wa Dawasco.

Akielezea juu ya mpango huo, Bw.Kaoneka alisema kwa kipindi cha miaka ya nyuma kiasi cha maji kilichokuwa kinazalishwa hakikuweza kukidhi mahitaji ya wananchi wote hususani wakazi wa ilala, hivyo kupelekea wengi kuchimba visima vya maji binafsi.

“Tulikuwa na changamoto ya utoshelezaji wa Maji kwa maeneo mengi ya mji. Uzalishaji Maji haukuwa mkubwa hivyo kwa wananchi wengi iliwalazimu kuchimba visima vyao binafsi ili wapate huduma hiyo”alisema meneja huyo.

Alitolea mfano maeneo mengi kwa mkoa wa Ilala yenye huduma ya Visima kwa watu binafsi ni maeneo ya Kariakoo, Upanga na katikati ya Mji.

“Kwa sasa uzalishaji wa Maji umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka kiasi cha lita za ujazo milioni 182 hadi lita za ujazo milioni 270 kwa siku, hivyo kupelekea maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam kuwa na utoshelezi mwingi wa Maji.

“Hivyo tutoe rai kwa wamiliki wote wa visima katikati ya mji kuja ofisi za Dawasco ili kujiunga rasmi na mtandao wa Majisafi. Tumekuja kugundua wengi wa wamiliki wa visima hufanya maunganisho ya Maji bila kufuata taratibu husika na mwisho hudai yale maji ni ya kisima wakati Dawasco tukishayapima tunagundua ni ya Dawasco” aliongeza Kaoneka.

Bw.Kaoneka alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wananchi wanaohujumu miundombinu hiyo kwa kupiga namba 0769 988 677 au 0743 451 879.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: