Picha : Mheshimiwa Rais Ellen Johnson, Mheshimiwa Raila Odinga na Mheshimiwa Rais mstaafu B.W.Mkapa na Mheshimiwa Mama Anna Mkapa nchini Nigeria.

Muda sio punde tukio la ufunguzi wa maktaba kubwa na ya kisasa ya aliyekuwa Rais wa Nigeria Mheshimiwa Olusegun Obasanjo imeanza na kwangu mimi kama mpenzi wa kuandika vitabu na utunzaji wa kumbukumbu hii ni kitu ambayo imenivutia na kunifanya niifuatilie kwa ukaribu.

Maktaba hiyo imebatizwa jina la Olusegun Obasanjo Presidential Library.

Ndugu yangu Madaraka Nyerere ataungana nami ya kuwa kama Taifa moja ya vitu ambavyo tunapaswa kutilia mkazo ni utunzaji wa kumbukumbu juu ya mambo mbali mbali katika maandishi kwa manufaa ya nchi na vizazi vijavyo viweze kuja kujua ni nini kilipata kutokea katika zama zetu / au mambo mbali mbali yalikwendaje.

Shime kwetu sote wana wa Tanzania, tupende KUANDIKA, KUSOMA, KUDADISI juu ya historia na mambo mbali mbali ambapo kwa kufanya hivyo tutaweza kuelimisha vizazi na vizazi.

Mtu mmoja aweza sema haya ya kwetu kwa wakati huo yatakuwa yamepitwa na wakati bila kujua kwa undani. Ngoja nikupe mifano :

- Ikiwa ni mpenzi wa fasheni au unajua kidogo sio ile kwa saaana kama dada yangu Maria Sarungi-Tsehai utagundua ya kuwa mitindo iliyowika zama zileee sasa inarudi kwenye chati .

- Ikiwa unafuatilia kwa undani juu ya namna mambo katika nchi kwa sasa yanaenda utapata kujua ya kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Azimio la Arusha ambalo muasisi wake ni hayati Mwl. Nyerere basi ikiwa hupendi kusikia kuhusu AZIMIO basi nikukumbushe ile kauli mbiu ya Kilimo kwanza ambayo Mh. Pinda aliisimamia kidete utajua ya kuwa muasisi wake ni Mwalimu Nyerere pia kupitia azimio lake la Siasa ni Kilimo .

Hayo yote ninayaandika ili tu niweze kuamsha ari ndani yako ewe rafiki yangu kipenzi ili walau ukiweza anza kununua na kutunza vitabu katika maktaba yako binafsi, andika vitabu , soma na kusimulia ama kuandika baadhi ya yale unayoyasoma.

Ni hayo tu, ili nisikuchoshe wacha nikutakie mapumziko mema ya mwisho wa juma yenye baraka na fanaka.

Asante.

@ BAGATECH

Godwin D. Msigwa
Dar es salaam
Tanzania
4 Machi 2017
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: