Thursday, April 27, 2017

BALOZI WA KUWAIT NCHINI MHE. JASEM AL-NAJEM AENDELIEA KUUNGA MKONO SHULE YA SEKONDARI YA TOLIDO

Ubalozi wa Kuwait unaendelea kuiunga mkono Shule ya Sekondari ya Tolido iliyopo Tanga kwa kuipatia idara ya shule hiyo mashine ya kutoa kopi (photocopy machine) iliyopokelewa na msimamizi wa Shule Bi, Basilisa Soka.

Mashine hiyo inatarajiwa kuisaidia Shule na kurahisisha kazi za idara kwa ajili ya kuinua kiwango cha elimu.

Itakumbukwa kuwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jasem Al-Najem alizindua kisima cha maji katika shule hiyo mwishoni mwa mwaka jana 2016 ambapo mradi wa ujenzi wake ulifadhiliwa na Msamaria mwema raia wa Kuwait na kutekelezwa na Asasi ya Direct Aid-ofisi ya Tanga, kisima hicho ndio cha kwanza kuzinduliwa tangu ubalozi wa Kuwait kuzindua mpango wake wa 'Kisima cha maji kwa kila Shule'.

Idadi ya visima ambavyo tayari vimezinduliwa ndani ya mpango huo vimefikia visima 27 katika shule mbalimbali katika kipindi cha miezi minne tu.

Ubalozi wa Kuwait utaendela kuisaidia Shule ya Tolido ya Sekondari mjini Tanga na shule nyingine Tanzania ili kuunga mkono mchakato wa elimu nchini.

1 comment :

Lelo said...

Tunawashukuru sana Balozi, ubalozi wa Kuwait pamoja na mkurugenzi wa African Muslim Agency Tanga kwa msaada wanaoutoa kusaidia shule ya secondary Toledo. Mungu awabariki sana.

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu