Mkuu wa Kitengo cha Masoko katikaka benki ya DTB, Nd. Sylvester, akiongea na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya New Afirica. Benki ya DTB Imetangaza faida kabla ya kodi ya Bilioni 30 katika mwaka wa biashara 2016.

Na Mwandishi Wetu.

Diamond Trust Bank Tanzania Limited (DTB) kwa mara nyingine imetangaza mafanikio katika taarifa ya kifedha ya mwaka 2016. Faida kabla ya kodi kwa mwaka 2016 imeongezeka kutoka shilingi bilioni 27.3 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 31.0 kwa 2016.

Amana za wateja za DTB zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 737 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 800 mwaka 2016. Jumla ya rasilimali za benki ni shilingi bilioni 984 mwaka 2016 ukilinganisha na shilingi bilioni 900 kwa mwaka 2015.

Mikopo kwa wateja imeongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 565 mwaka 2016 toka shilingi bilioni 536 kwa mwaka 2015. DTB Tanzania vile imeendelea kuthibiti mikopo isiyolipika na kubaki chini ya 3% ukilinganisha na 9.5% ya sekta ya benki.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko katikaka benki ya DTB, Nd. Sylvester, akiongea na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya New Afirica. Benki ya DTB Imetangaza faida kabla ya kodi ya Bilioni 30 katika mwaka wa biashara 2016.katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Nd. Viju Cherian na kushoto ni mkuu wa kitengo cha Fedha, Nd. Joseph Mabusi.

Akiongea na wanahabari Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Ndugu Viju Cherian alisema kwamba, “Ongezeko la faida kwa DTB Tanzania, hasa kwa mwaka 2016 ambapo benki nyingi zimekua kwa kiwango kidogo ni ushuhuda tosha wa muundo wa DTB Tanzania wa kihafidhina ulio na ufanisi wa hali ya juu. “Alisema pia “Utekelezaji wa mpango mkakati wao wa mwaka 2008 ulioifanikisha DTB Tanzania kufungua matawi 20 ndani ya miaka minane ni jambo ambalo limechangia katika kukuza amana za wateja na kutuwezehsa kutoa mikopo kwa riba nafuu zaidi.

Huduma bora kwa wateja,mtandao wa matawi pamoja na bidhaa bora zinazokidhi mahitaji ya kila aina ya mteja ni sifa zilizopelekea ukuaji wa DTB Tanzania kwa mwaka 2016. “DTB Tanzania haina mpinzani katika kutoa huduma bora na kutekeleza mahitaji ya mteja. Tunaendelea kuwa wabunifu na kuwekeza kwenye teknolojia kama njia ambayo itatuwezesha kuwa karibu zaidi yateja wetu.” Aliongeza Ndugu Cherian.

Mwaka 2016 DTB Tanzania ilifunfua matawi mawili jijini Dar es Salaam na kifuikisha matawi 11 jijini Dar es Salaam na jumla ya matawi 26 nchi nzima. Tawi la CBD (Central Business District) kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Mirambo katika jengo la Diamond Plaza lilifunguliwa Machi 2016 na Tawi la Mbezi Chini lililoko Mbezi Beach katika kata ya Kawe lilifunguliwa Octoba 2016. Malengo ya DTB Tanzania kwa mwaka 2017 ni kufungua matawi yasio pungua manne ifikapo Disemba. Matawi ambayo yako kwenye mpango wa kufunguliwa hivi karibuni ni pamoja na Tawi la Uhuru, Kariakoo na Tawi la Mlimani City, Mwenge.

Katika kutambua ukubwa wa Tanzania kijiografia na haja ya kutaka kufikia wateja wengi zaidi DTB Tanzania imeanza mchakato wa kuwekeza katika mradi wa kuanzisha huduma ya kupitia mawakala. Huduma hii itaongeza wigo wa DTB Tanzania si mjini tu bali hata vijijini ambako benki nyingi hazijaweza kufika huku ikiwasogeza Watanzania huduma za kifedha karibu zaidi.Huduma hii inatarajiwa kuanza ndani ya nusu ya pili yam waka 2017.

DTB Tanzania pia imeendelea kupiga hatua kiteknolojia kwa kuboresha mfumo wake wa kibenki na kuja na mfumo wa Flex Cube V12.0 ambao una uwezo wa kiutendaji zaidi kutokana na mahitaji. Huduma ya DTB Mobile Banking ijulikanayo kama Touch 24/7 pia imeboreshwa na sasa mteja anaweza kufanya miamala ya kibenki popote alipo. iBank ambayo ni huduma ya benki hiyo kupitia mtandao wa intanetia pia imeboreshwa katika hali ya kumridhisha mteja zaidi.

Mtandao wa matawi ya DTB Tanzania ni kama ifuatavyo, Dar es Salaam: (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, Nyerere, Kariakoo, barabara ya Nelson Mandela karibu na makutano ya Tabata, Upanga barabara ya Umoja Wa Mataifa, CBD kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Mirambo na Mbezi Chini Kawe. Matawi mengine ni pamoja na Arusha (2), Mwanza (2) na tawi moja katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora, Tanga na Zanzibar.

DTB Tanzania ni sehemu ya DTB Group, ikiwa na matawi zaidi ya 130 katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi. DTB Tanzania pia ni mshirika wa Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED), mkono wa maendeleo ya kiuchumi wa Mfuko wa Kimaendeleo wa Aga Khan.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: