Na Ruhinda Franco, Dar es Salaam.

Nchi nyingi zilizoendelea huwalipa wafanyakazi kwa saa na wengine kwa siku. Wanafanya hivi kwa sababu malipo yanategemea na UZALISHAJI kwa muda fulani. Hii inamanisha Kama Huwezi kuzalisha siku hiyo Huwezi kupata fedha yoyote maana hujafanya kazi.

Hapa kwetu Tanzania malipo ya mfanyakazi ni kwa mwezi. Mfumo huu wa malipo japo unapendwa na watu wengi lakini nimegundua kuwa ni Mfumo mbaya sana kwa sababu Zifuatazo :

*1.Huwafanya watu kuwa wavivu*

Kulipwa mshahara mwisho wa mwezi kumesababisha kuwepo kwa watu wengi kufanya kazi kivivu Huku wakisubiri mshahara mwisho wa mwezi haijalishi wamezalisha kiasi gani.

Hali hii imetengeneza watu wavivu ambao Huwa wanatengeneza hata sababu za kutokwenda kazini maana mshahara upo pale pale.

Kama ingekuwa kulipwa kwa siku tungetengeneza watu wanaotunza muda na kutumia muda mwingi kuzalisha kuliko kuchat na kupiga story kazini.

*2.Huwafanya watu kuwa maskini bila kujua*

Ukiwa kwa mwezi unalipwa 600,000 maana yake kwa siku unalipwa 600,000/30 sawa na sh 20,000/= .

Sh. 20,000/= ni sawa na Mjasiriamali aliyeamua kujikita kwenye biashara ya kuuza chapati ambapo akiuza chapati Mia hupata 20,000/= na huuza kuanzia saa Moja mpaka saa nne tu na baadae kwenda kwenye shughuli zake. Huyu anayelipwa 20,000/= kwa masaa kumi maana yake kila saa analipwa sh elfu mbili (2,000/=).

Sasa kwa sababu waajiri hawataki ujue Kama unalipwa 1000 kwa saa kwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi na elfu mbili kwa mshahara wa laki sita, wanaamua kuficha hili na kulipa mshahara mwisho wa mwezi.

*Jambo la msingi*

Mshahara usikupe kiburi yawezekana unalipwa Mia tano kwa saa. Je kwa saa huwezi kuzalisha zaidi ya elfu mbili ukiamua ✍✍??

Watch out.....
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: