Sunday, April 30, 2017

KIJANA ALIYETOKA DAR HADI ARUSHA KWA BAISKELI AZINDUA KITABU CHAKE

Pichani ni Mwandishi wa kitabu hicho Wiseman Luvanda, Akizungumza na baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo jana Jijini Arusha. Picha na msumbanews blog
Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu akipokea kitabu kutoka kwa Mwandishi Wiseman Luvanda.Picha na msumbanews blog
Baadhi ya wadau mbali waliojitokeza kwenye kongamano la kuinuliwa viwango na uzinduzi wa kitabu hicho.
Mwandishi Wiseman Luvanda akifuatilia kwa makini kongamano la kuinuliwa viwango ambalo lilifuatana na uzinduzi wa kitabu chake.

Mheshimiwa Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu , jana amezindua rasmi kitabu cha " KUKIWA NA FOLENI" kilichoandikwa na Wiseman Luvanda.

Pia Nabii Dr.GeorDavie alimpongeza kwa kitendo chake alichoamua kufanya kwa kuwa balozi wa barabarani kwa kutoka Jijini Dar es salaam hadi mkaoni Arusha wa usafiri wa baiskeli.

Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo mtunzi wa kitabu hicho alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu na si kulalamika kila siku, jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.

Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha " KUKIWA NA FOLENI" , ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kukisambaza nchi nzima.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu