Kama ilivyoaada kwa wasomaji wote wa Kajunason Blog ni kujuliana hali pamoja na kuweza kuwapa habari moto moto kutoka pande za dunia.

Pamoja inapenda kuwatakia  HERI YA PASAKA!!! Heri ya Pasaka

Pasaka ni siku muhimu sana hasa kwa wakristo ambapo wanasherehekea ufufuko wa bwana Yesu kristo baada ya mateso, na hii huashilia ukombozi wa mwanadamu.

Tunawaomba msherehekee kwa AMANI kabisa ili baada ya sherehe hizi tuendelee na maisha kama kawaida.

ANGALIZO.

1. Epuka kunywa pombe kupita kiasi wakati huu, maana inaweza ikakupelekea kupata madhara ambayo utakuja kujuta maisha yako yote.  Kuna watu huwa wanabadilika na kuwa na ulemavu wa kudumu baada ya kupata ajali kwa sababu ya ulevi, jilinde na uwalinde wenzako pia.

2. Epuka kwenda katika nyumba za starehe, ni hatari sana hasa nyakati za usiku. Nenda mchana na familia yako, usiku uwe nyumbani, kwa kufanya hivo utakuwa umeulinda mwili wako na wenzako pia.

3. Epuka matumizi ya pesa yasiyo ya lazima katika sikukuu hii. Mambo ya msingi ni kununua chakula chako na familia yako, si kulewa na kutoa ofa zisizo na msingi wowote. Epuka matumizi hayo kwani kesho utakuwa unajuta kwa kutumia pesa nyingi nje ya bajeti. Ukiweza kujicontrol kwa hili basi maisha yako yanaenda kubadilika.

Hayo ndo niliyojaliwa kukushauri wewe ndugu yangu ili ufanye maamuzi ya busara ili usije ukajuta. 

Wenu 

Cathbert Angelo Kajuna,
Mkurugenzi Mtendaji,
Kajunason Blog.
16.04.2017.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: