Thursday, April 27, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika gari maalum na kuwapungia mkono Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakati wa sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeho.
Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, pamoja na Wananchi mbali mbali  wa Mji wa Dodoma wakiwa katika Uwanja wa Jamhuri,wakati wa sherehe za  maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo, Mgeni  rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya  Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Uhuru zilizofanyika leo, ambapo  Mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume pamoja na mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono ya pongezi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na walioshiriki katika zoezi la kuchanganya udongo kuasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Wananchi hao ni Bw. Hassan Omary Mzee (hayupo pichani), Bw. Hassaniel Elisael Mrema (kushoto), Bi. Sifael Kunda Shuma (anayepewa mkono) na Bi. Khadija Abbas Rashid
Gadi ya “Komando” la vijana likiwajibika kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Onesho la ndege vita kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Onesho la mbwa wa polisi kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Onesho la Komandoo wawili kuvuta lori la tani 7 kwa mikono kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kikosi cha Komandoo cha JWTZ kikitoa heshima kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu